Sunday, 14 July 2019

TCRA KANDA YA KASKAZINI YAFANYA MKUTANO NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI

Mwenyekiti  wa Kamati ya Maudhui mamlaka ya mawasiliano TCRA Valerie Msoka akizungumza na washiriki ambao ni waandshi ya habari juu ya kutoa taarifa zenye weledi na usawa kwa jamiii
Afisa Mawasiliano Makao Makuu TCRA  Rolf Kibanja akitoa elimu kwa washiriki  walio hudhuria mkutano huo katika ofisi za mkuu wa wilaya ya Arusha mkoani Arusha.
Pichani ikionyeshaa washiriki waliohudhulia mkutano wakinakili kinacho fundishwaa na bodi  ya Mamlaka ya Mawasiliano.

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA )Kanda ya kaskazini wamefanya mkutano kwa wamiliki wa vyombo vya habari,watangazaji,wahariri katika mkoa wa Aarusha lengo likiwa ni kuwapa elimu waaandishi ya habari kutumia kalamu zao kuandika taarifa zenye usawa na haki katika  jamii bila kuweka upendeleo wowote hususani katika kipindi cha uchaguzi  

Valerie Msoka ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui(TCRA) akizungumza na waandishi habari wa vyombo vya habari tofauti katika mkoa wa arusha  amesema lengo la mkutano huo wa waandishi ni kutoa elimu ya kuandika taarifa zenye usawa na haki katika jamii pamoja na kujadili changamoto zinazo ikumba tasnia ya habari mkoani arusha 

 Mwenyekiti huyo wa Maudhui (TCRA) amesema zipo changamoto nyingi zina zoikumba tasnia ya habari nchini ikiwemo wamiliki wa vyombo vya habari kuingilia  ujuzi wa waandishi wa habari kwa lazimisha kufanya jambo kinyume na sheria za vyombo vya habari
 Anasema

Licha ya changamoto nyingi ambazo waandishi wa habari wanazopitia lakini moja ya changamoto kubwa sana ambazo sehemu nyingi tulizo pitia waandishi wa habari wanadai wamili wa vyombo vya habari kuwaingilia katika majukumu yao jambo ambalo lina wafanya kuandisha habari zilizo egemea sehemu moja”Alisema .

 Vile vile  Kaimu mkuu wa  Mamlaka ya Mawasiliano kanda ya Kaskazini Imelda Salum amesema Mamlaka imeweka mikakati mingi ya kuboresha Tasnia ya habari kanda ya kaskazini na moja ya mikakatin ilio weka na mamlaka iyo ni kuwapa elimu waandishi wa habari ili kuandika taarifa zenye usawa na ukweli huku akiwataka waandiishi wa habari wasinyamaze pindi watakapoona na kusikia taarifa zozote za upotoshwaji.

Nao washiriki waliohudhulia mkutano huo wameishukuru mamlaka ya mawasiliano kanda ya kaskazini kwa kuwapa elimu hio kwani imewapa uelewa wa mambo mengi huku wakiomba mamlaka hio  kuboresha njia za upatikanaji wa habari kwa njia rahisi.

Mwisho

No comments:

Post a Comment