Wajumbe wa UVCCM wakiwa wamembeba Mwenyekiti mpya wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi  mkoa wa Arusha Omary  Lumato mara baada ya kutangazwa mshindi .


Mwenyekiti mpya wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Omary Bahati Lumato,amesema kuwa kipaumbele chake ambacho amekipanga kuanza nacho katika kipindi cha uongozi wake kuyafuta makundi yote yaliopo ndani ya umoja huo pamoja na chama hicho ndani ya mkoa wa huo na atanje ili kuwafanya wanaccm wote kuwa wamoja.

Aliyabainisha hayo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa CCM mkoa uliopo jijini hapa mara baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo ya umwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha ambapo aliibuka kidedea kwa kupata kura 221,huku mgombea wa pili ambaye ni Suleman Msuya akipata kura 199 na mgombea wa tatu akiambulia kura 7 huku vijana ambao ni wajumbe waliojitokeza kushiriki zoezi hilo wakiwa 447 .

Aidha akiongea mara baada ya kutangazwa alisema kazi ya kwanza atakayofanya ni kuvunja makundi yote yaliopo ndani ya chama hicho ,ili kufanya wanachama wote kuwa wamoja na alibainisha kuwa anaamini wakiwa wamoja majimbo yote ya Arusha ambayo yanaongozwa na upinzani yatarudi kumilikiwa na chama cha mapinduzi na sio kurudishwa tu CCM bali Arusha itakuwa ngome ya chama hicho.

"nashukuruni sana kwa kunichagua na kuanzia sasa natangaza rasmi nimevunja makundi yote ,namimi ni kiongozi wa vijana wote na sio wa kundi lolote,nanyie vijana napenda kuwaambia ili tumiliki aya majimbo yote pamoja Arusha tumechukua sehemu mbalimbali ukiangalia kata nyingi zimerudi ccm kwani madiwani wao wamejiuzuru na kurudi chama tawala na kurudi huku kwa hawa ni salamu tosha kwa wapinzani kuwa hawana kitu hapa "alisema Omary 

Alibainisha kuwa tabia ya makundi inatakiwa kpigwe vita vikali na iachwe mara moja ili ushinde wa uchaguzi zijazo kuanzia serikali za mitaa hadi uchaguzi mkuu ushindi uwe wa CCM huku akibainisha kuwa mtu ambaye anaendekeza na kuendelea kuwa na makundi huyo atakuwa msaliti wa chama hicho na hafai kuwa kiongozi wala mwanachama wa chama hicho.

Kwa upande msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mbunge wa Mtera pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM Livingstone Lusinde alisema kuwa wanawapongeza sana vijana wamefanya uchaguzi kwa amani pia alisema anawapongeza sana wagombea kwani wakati kila mgombea mmoja alipokuwa anajinadi alikuwa anaongelea kuvunja makundi hivyo anawapongeza zaidi kwani vijana wa Arusha wamejifunza na wamejua ni kitu gani kilichokuwa kinafanya majimbo kupotea na kwenda kwa wapinzani .

"nawapongeza vijana wa Arusha kwakuwa vijana wamejitambua na wamejua hatukua tunashidwa uchaguzi wowote bali makundi ndio yanawamaliza na wameahidi kuvunja makundi yao ,naunajua amna uchaguzi bila makundi bali makundi hayo yanatakiwa yavunjwe tu mara baada ya uchaguzi kuisha na tumeona hapa vijana wameyavunja mapema makundi hayo na wametangaza hatharani hivyo napenda sana kuwapongeza"alisema Livingstone

Amewahimiza kuhakikisha wanahamasisha Vijana na wanachama wa ccm kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kwenye serikali za mitaa huku akisisitiza kuwa Vijana wanao wajibu kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinaibuka mshindi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Lusinde, ambae ni mbunge wa jimbo la Mtera mkoani Dodoma, amewataka Umoja wa Vijana kuhakikisha wanahamasisha Vijana na wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakao fanyika nchini kote mwaka huu

Akitoa shukrani zake kwa vijana mmoja wawagombea hao Suleman Msuya alishukuru wajumbe wa vijana hao kwa kushiriki zoezi hilo na kusema kuwa amekubaliana na matokeo na kuahidi kuendelea kumuunga mkono Mwenyekiti mpya alieshinda ,huku akiwasisitiza vijana kuvunja makundi ambayo wanayo ili kujenga CCM moja yenye nguvu.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: