William Ole Nasha Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Ngorongoro akizungumza na wananchi na Wafugaji katika tarafa ya Ngorongoro.
 James Ole Millya Mbunge wa Simajiro amesema kuwa uwezweshaji wa kundi la wafugaji wanaoshi katika mamlaka hiyo utasaidia pia katika kuiua vyanzo vipya vya mapato
William Ole Nasha ni Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Monduli,James Ole Millya ni Mbunge wa Simajiro,Amina Mollel ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha,Mbunge wa Monduli kama wanavyoonekana katika picha.

Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wafugaji katika tarafa ya Ngorongoro wakishirikiana na Viongozi wa kisiasa na taasisi za umma na binafsi wamekusanya kiasi cha shilingi milioni 125 ambazo zitatumika kuimarisha vikundi vya kuweka akiba na kukopa (Vikoba )  ili kusaidia kaya masikini kujikwamua kiuchumi.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Edward Maura amesema kuwa wafugaji kutoka vijiji vya tarafa ya ngorongoro wamekutana na kuanza kuchanga zaidi ya shilingi milioni miamoja  huku wengine wakijitolea mbuzi ng’ombe na kondoo ambapo mwenyekiti wa baraza la wafugaji ngorongoro edward maura anasema wafikika hatua hiyo baada ya kutafakari na kuona kuwa hakuna sababu ya kusubiri misaada kutoka nje wakati wenyewe wanauwezo wa kutatua changamoto zao kwa kuunganisha nguvu pamoja.
Mbunge wa Ngorongoro William Ole Nasha amesema kuwa hatua ya kusaidia vikundi hivyo itasaidia katika kupunguza umasikini kwa wafugaji hao kwa kutumia Vikoba ambavyo vimekua vikileta matokeo makubwa katika uchumi wa wananchi.
Naye Mbunge wa Simajiro James Ole Millya amesema kuwa uwezweshaji wa kundi la wafugaji wanaoshi katika mamlaka hiyo utasaidia pia katika kuibua vyanzo vipya vya mapato mbali na mifugo na pia na pia kuona umuhimu wa kuhifadhi rasilimali za wanyamapori na mazingira.
“Wafugaji wamekua wahifadhi wakubwa katika maeneo ya hifadhi hivyo wanapaswa kuthamaniwa na kuwezeshwa kiuchumi ili waone matunda ya uhifadhi” Alisema Millya
Hata hivyo Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha amina Mollel amesema kuwa juhudi za kuwawezesha wanawake kwa njia ya mikopo yenye riba nafuu zinapaswa kupewa kipaumbele na serikali imekua ikitoa fedha hizo za asilimia 10% kwa wanawake na vijana .
Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro eneo wanaloishi wafugaji hao Profesa  Abiudi  Kaswamila anasema mpango huo utaleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa jamii hiyo.
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: