Mbunge wa Viti Maalum anaewakilisha Vijana mkoani Dodoma, Mariam Ditopile ametekeleza ahadi yake ya kuchimba kisima kwa wananchi wa eneo la Mkoka Jimbo la Kongwa chenye uwezo wa kutoa Lita 25000 kwa saa.
Mariam amekabidhi kisima hicho kwa wananchi wa Kongwa mbele ya Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Spika wa Bunge, Mhe Job Ndugai.

"Niliahidi kuchimba kisima kwenu ndugu zangu wa Kongwa, sisi kama wasaidizi wa Rais Magufuli tunapaswa kuhakikisha tunamsaidia Rais wetu ambaye ameuletea Maendeleo Mkoa wetu wa Dodoma.”
“Tunapaswa kumuunga mkono kwa vitendo katika kuwatumikia wananchi wanyonge ambao Rais wetu amekua akiwapigania kila siku," amesema Ditopile.

Kwa upande wake Spika wa Bunge, Job Ndugai amempongeza Ditopile kwa namna ambavyo amekua akiwatumikia wananchi wa Dodoma huku akimtaka kutosita kuongeza nguvu katika sekta zingine ikiwemo Afya na Elimu.
" Mimi sina shaka na Ditopile, huyu ni kijana ambaye amekua akitoa ahadi na kutimiza, hivi karibuni alitoa ahadi ya kusomesha wasichana watakaofaulu kwenda kidato cha tano na ametimiza, hivyo nimpongeze na nimtie moyo katika kuwatumikia wananchi wa Dodoma," amesema Spika Ndugai.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: