Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana akionyesha bunduki aina ya Ak -47  pamoja na risasi 20 zilizokamatwa jana katika misitu ya milima ya Digodigo  Tarafa ya Sale wilaya ya Ngoronroro.

Na Vero Ignatus,Arusha

Watu wawili wanaosadikiwa  kuwa majambazi wameuwawa katika majibizano polisi eneo la Digodigo ,Tarafa ya Sale Wilayani Ngorongoro

Akizungumza na waandishi wa habari jana , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana alisema ,majambazi hayo yalikuwa na bunduki aina ya Ak -47  pamoja na risasi 20

Amesema majibizano hayo yalichukua zaidi ya dakika 75 huku wenyeji wakishuhudia mirindimo ya risasi ambapo tukio hilo liketokea jana saa 3:00 asubuhi kwenye msitu wa Digodigo Tarafa ya Sale Wilayani Ngorongoro

Aliwataja waliokufa  kuwa ni Kulima Albart (35) mkazi wa kijiji cha Mholo  na Hashim Nginodya(28)mkazi wa Digodigo ambapo miili yao umehifadhiwa hospitali ya Digodigo

Amesema watu hao wanaosadikiwa ni majambazi walikuwa wakitafutwa muda mrefu kwa matukio ya unyang'anyi na kuteka watalii

"Majibizano ya risasi yalichukua dakika 75 pia baada ya majibizano walikutwa na risasi 20  pamoja na bunduki aina ya Ak-47"

Sambamba na hayo Kamanda  Shana amesisitiza kuwalinda wafanyabishara wote wa Mkoa wa Arusha na kutoa rai walipe kodi ikiwemo kufuata taratibu za kisheria zilizopo katika kufanya shuguli zao

Natoa onyo kali kwa wale wote wakwepa kodi kuhakikisha wanaliodi ili wasije kukumbana na mkono wa serikali

Mwisho
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: