Thursday, 13 June 2019

RC Dodoma apiga marufuku shughuli za Kilimo kwenye vyanzo vya maji


Na Enock Magali,Chemba Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amepiga marufuku wananchi kufanya shughuli za kilimo na nyinginezo katika maeneo ya vyanzo vya maji.

Dkt. Mahenge ametoa katazo hilo mara baada ya kutembelea miradi miwili ya maji iliyopo katika kata ya Mondo wilaya ya Chemba mkoani Dodoma yenye thamanani ya zaidi ya Shilingi Milioni 900.

Akizungumza kwa nyakati fotauti wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika kijiji cha Mondo na kijiji cha Daki wilayani hapo, Dk Mahenge alisema lengo la Serikali ni kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama.

“Vyanzo vya maji vinatakiwa kutunza ili viwe endelevu, itakuwa haina maana ya uwekezaji wa miradi hii alafu wananchi wanakosa maji kutokana na uharibufu wa mazingira, ni lazima tutunze mazingira yetu ili nayo yatupatie mambo mazuri,” alisema Dk Mahenge.

Akizungumzia miradi hiyo mhandisi wa maji wilaya Robert Mganga alisema mradi wa maji katika kijiji cha Mondo una thamani na Sh673 milioni na unategemewa kuwafikia wakazi zaidi ya 4731 wa kijiji hicho pamoja na vijiji vinavyouzunguka.

Mganga alisema ujenzi huo umehusisha matanki mawili moja likiwa na ujazo wa lita 100,000 na jingine la lita 50,000 ya kuvuna maji ya mvua kutoka shule ya sekondari ya Mondo ambapo katika mradi huo utakuwa na vituo 14 vya kuchotea maji,, ujenzi wa nyumba ya mlinzi, pamoja na vitu vingine.

Ujenzi wa mradi huo ulianza Oktoba 2017 na ulitarajiwa kukamilika Februari 2018 lakini kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa fedha mradi huo haukukamilika kwa wakati.
Hata hivyo alisema kampuni inayotekeleza mradio huo ni Iwawa civil and building contractor limited ya Morogoro na iliomba kuongezewa muda hadi Mei 31, 2019 ambapo hadi sasa mkandarasi amekwishapatiwa kiasi cha zaidi ya Sh296 milioni.

Akizungumzia kuhusu mradi wa wa maji kijiji cha Daki, Mganga alisema unagharimu kiasi cha zaidi ya Sh359 milioni na kuhudumia wakazi zaidi ya 1201 wa kijiji hicho.

Mganga alisema mradi huo unatekelezwa na kampuni ya  Kharton traders limited ya Dar es salaam na umefika katika hatua ya umaliziaji huku akisema miradi hiyo inatakiwa kukamilika mapema ili wananchi wote wanufaike na huduma hiyo.

Alisema kukamilika kwa miradi hiyo unawafanya wananchi kutumia muda mwingi kwenye shughuli za maaendele na uzalishaji badala ya kutafuta maji kama ilivyokuwa  kipindi kilichopita.

Awali wananchi hao akiwemo mwalimu wa shule ya msingi Mondo Ester Msemo alishukuru Serikali kuwafikishia huduma ya maji katika kijiji hicho akisima awali walikuwa wakitumia maji ambayo si safi na salama.

No comments:

Post a comment