Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi amempa siku sita mkandarasi anaesimamia ujenzi wa mradi wa maji Kongwa kuhakikisha anarudia kulimaarisha tenki ambalo limeanza kuvuja angali bado jipya.

" Nimefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa kutembelea mradi wa maji Kongwa na mradi wa Machenje. Katika mradi wa Kongwa wenye thamani ya 1.5 Bilioni tumebaini mapungufu mengi na hivyo nimempa mkandarasi siku sita kazi ziwe zimekamilika laasivyo tutamchukulia hatua.

" Katika mradi wa Machenje wenye thamani ya Milioni 700, nimemuagiza Mhandisi wa Maji Wilaya amuite mkandarasi ofisini atupe majibu kwanini toka kukamilika kwa mradi huo pump imepungua mara mbili na wananchi bado hawapati maji. Lengo letu ni kuhakika tatizo la maji linakwisha kabisa Kongwa," amesema DC Ndejembi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: