Na Lucas Myovela

Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa amewaondoa hofu waliyo kuwa wamiliki na wafanyabiashara ya kubadili fedha za kigeni (bureau de change) hapa nchi na kuwahakikishia serikali kuja na mikakati imara dhidi ya biashara hizo za kubadili fedha za kigeni hapa nchini kwa maneno yenye mipango mkakati na kusajili maduka maalum yatakayo kuwa yanafaamika kiserikali na kupewa usajili ili kuondoa biasha holela ya kubadilisha fedha za kigeni.


Waziri mkuu ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa 24 wa wanahisa wa benki ya CRDB hapa nchini mkutano unaofanyika jijini Arusha kwa siku mbili mfululizo huku lengo kuu la mkutano huo likiwa ni kukuza uchumi wa nchi kufikia tanzania ya viwanda na uchumi wa kati kwa wanachama na wanahisa wa benki hiyo hapa nchini na kuzitaka taasisi za kifedha kutoa elimu ya mikopo kwa wateja wao.


Majaliwa alisema serikali iliamua kufungia bureau de change zote hapa nchini lengo likiwa ni kuzihakiki taasisi hizo za kubadili fedha za kigeni kutoka na bureau de change nyingi zilikuwa zikijiendesha kinyemera na kukwepa ulipaji wa kodi kitu ambacho kilisababishia hasara kubwa kwa taifa na kufanya taasisi rasmi za kifedha kukosa soko husika kulingana na viwango vilivyo pangwa na benki kuu ya Tanzania ( B.O.T.) na ameweza kuipongeza bank ya CRDB kwa kusimamia vyema ubadilishaji wa fedha za kigeni kwani ndiyo bank inayo ongoza kuliko mabank mengine katika biashara ya kubadilisha fedha za kigeni.


Aidha waziri mkuu kasimu majaliwa amewataka viongozi wa taasisi za hapa nchini kuwajibika kikamilifu katika utoaji wa huduma kwa wananchi na kuhakikisha huduma zinawafikia kirahisi wananchi na wanachama wao popote walipo na kwa wakati kwani kumekuwa na wimbi kubwa la viongozi wengi hapa nchini kutokuwa na uwajibikaji na maadili mema katika maeneo yao ya kazi kitu kinacho changia uporomokaji wa maadili pamoja na ufanisi katika taasisi nyingi.


Nae kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa benki ya CRDB  hapa nchini Bw Abdulmajid Nsekela ameeleza kwamba mpaka sasa hisa za  benki hiyo CRDB zinamilikiwa na wananchi pamoja na serikali kwa asilikia 90 na mpaka sasa CRDB inamatawi zaidi ya 263 nchini kote na tayari mipango mikakati imeshawekwa ili kuhakikisha wanazidi kupanua matawi zaidi na kutoa huduma bora zaidi na zenye kustahili zinazo endana na bank hiyo.


Aidha Nsekela ameleza kwamba taifa la Tanzania linahitaji taasiai imara za kifeza ili kuweza kukuza ustawi wa taifa kiuchumi na kuunga juhudi za Rais wa Magufuli kwa kufikia uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda na kuiomba serikali kuongeza kwenye mitahara ya elimu juu ya maswala ya hisa na uwekezaji wake katika taasisi mbalimbali ili kujenga uweledi bora na ufahamu wa hisa kwa watanzania wengi kitu ambacho kitasaidia ukuachi wa uchumi kwa kasi.


Awali mkurugenzi wa TRA hapa nchini Charlse Kichele akisoma hotuba ya waziri wa Fedha  Dk Philip Mpango ambapo aliweza kumuwakilisha alieza kuwa kupita
Share To:

msumbanews

Post A Comment: