Watu 41 wameuawa baada ya ndege ya Urusi kutua kwa dharura na kulipuka moto katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo mjini Moscow.

Video katika mitandoa ya kijamii zinaonyesha baadhi ya abiria wakitumia mlango wa dharura na kutoka kwenye ndege hiyo ya Aeroflot iliyokuwa inateketea moto.

Watoto wawili na mhudumu mmoja ni miongoni mwa waliofariki kwa mujibu wa vyombo vya habari Urusi.

Shahidi mmoja amesema ilikuwa ni "miujiza" kwamba kuna aliyenusurika mkasa huo wa ndege, iliyokuwa imebeba abiria 73 na maafisa watano wa ndege.

"Watu 37 wamenusurika - Abiria 33 na maafisa wanne wa ndege hiyo," amesema afisa wa kamati ya uchunguzi, Yelena Markovskaya.

Aeroflot, shirika la ndege la kitaifa Urusi limesema ndege hiyo ililazimika kurudi katika uwanja wa ndege " kutokana na sababu za kiufundi", lakini halikufafanua zaidi.

Ndege hiyo aina ya Sukhoi Superjet-100, iliondoka uwanja wa ndege wa Sheremetyevo mwendo wa saa 18:02 kwa saa ya huko kutoka eneo la Murmansk.

Maafisa wa ndege wakatoa tahadhari ya wasiwasi wakati kulishuhudiwa " hitilafu" muda mfupi baada ya ndege kuondoka.

Baada ya kutuwa kwa dharurua katika uwanja huo wa ndege , injini za ndege hiyo ziliwaka moto katika njia kuu wa ndege, Aeroflot limesema katika taarifa.

Maafisa hao wa ndege "walijitahidi kadri ya uwezo wao kuwaokoa abiria ," waliofanikiwa kutolewa katika muda wa sekundi 55, shirika hilo la ndege limeeleza
 
Kaimu Gavana wa mji eneo hilo la Murmansk, Andrey Chibis inaarifiwa amesema familia za waliofariki katika mkasa huo watalipwa $15,300 kola mmoja, huku waathirikwa watatibiwa katika hospitali na watapewa $7,650 kila mmoja..
Share To:

msumbanews

Post A Comment: