Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali,
Jimmy Matamwe, (Wa kwanza kulia) na Mwanasheria wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, Luteni Kanali, Godwill Benda pamoja na Mwanasheria wa Wizara ya
Mambo ya Ndani, Inspekta. William Mkamba, wakifuatilia mkutano wa kujadili
masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, Jijini
Arusha tarehe 31, Juni, 2019.
Mtaalamu anayeshughulikia masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya, Jacob Lusekelo,akifafanua masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hivyo, Jijini Arusha tarehe 31, Juni, 2019.
Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu, wanyamapori, Mifugo na Mazingira pamoja na wanasheria wa sekta hizo wakifuatilia mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Arusha tarehe 31, Juni, 2019.
Mwanasheria kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Wa kwanza kulia), Mhe. Verynice Kawiche, na Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mhe. Gilbert Ndeoruo, (katikati) pamoja na Mwanasheria wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Merick Luvinga, wakifuatilia mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Arusha tarehe 31, Juni, 2019.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe, (walio kaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu, wanyamapori, Mifugo na Mazingira pamoja na wanasheria wa sekta hizo wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Arusha tarehe 31, Juni, 2019

Na. OWM, ARUSHA
Wataalam wa sheria kutoka katika sekta ya
Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameshauri kutungwa
kwa sheria mpya itakayohusika na ulinzi
na usalama wa vimelea hatarishi ili kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama
wa sampuli za vimelea hivyo kutoweza kueeneza magonjwa kwa
binadamu.
Sheria hiyo imeshauriwa kuzingatia dhana ya
Afya moja ambayo hujikita katika kujumuisha
sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa
yanayomuathiri binadamu, lengo nikusaidia katika kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa kuvichukua vimelea kwa wanyama, binadamu na mimea
au wakati wa kuvisafirisha na kuvipeleka maabara kwa ajili ya
Uchunguzi na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti wakati wa
mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Ulinzi na Usalama wa vimelea
hatarishi, uliofanyika kwa siku tatu na kufungwa leo tarehe 31 Juni,
2019, Jijini Arusha, kwa pamoja, wataalam wa sekta za Afya na
wanasheria wa sekta hizo wamebainisha kuwa
uwepo wa sheria hiyo utasaidia kuimarisha usalama na ulinzi kwa
wanaohusika na shughuli za
vimelea hivyo, mafunzo kwa wataalamu hao, miundo mbinu ya maabara,
pamoja na kuainisha orodha ya vimelea
hivyo.
Wataalamu wa sekta za Afya
walioshiriki mkutano huo, wamebainisha kuwa, sheria hiyo ni ya muhimu kwa
kuzingatia kuwa, Dunia imekuwa na tishio kubwa la magonjwa ya kuambukiza
yanayoweza kusambaa kwa muda mfupi na kusababisha madhara makubwa kwa binadamu,
mifugo, wanyama pori na kuleta uharibifu wa mazingira. Wamefafanua kuwa, Tafiti zinabainisha kuwa kila mwaka huibuka
magonjwa ambukizi mapya kati ya matano hadi Nane duniani. Hivyo inakadiriwa
ifikapo mwaka 2030, dunia itakuwa na magonjwa ambukizi mapya 30.
Aidha, wamebainisha
kuwa, Tafiti mbalimbali duniani zinaonesha
pia, kuwa asilimia 60% ya vimelea vya magonjwa ambayo huambukizwa binadamu
vinatoka kwa wanyama hususani wanyamapori na baadae kusababisha
magonjwa kwa binadamu.Tayari Tanzania kupitia Dhana ya Afya Moja, imeainisha magonjwa sita ya kupewa kipaumbele
ambayo ni; Kimeta, Kichaa cha mbwa, Mafua ya ndege, Homa ya Bonde la ufa,
Malale na Ugonjwa wa kutupa mimba wanyama.
Akiongea wakati wa akifunga
mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy
Matamwe amebainisha kuwa serikali imedhamiria kuijenga jamii ya watanzania yenye Afya bora
kwa kuikinga na majanga yatokanayo na magonjwa ya mlipuko, hivyo ushauri huo
wa wanasheria na wataalam wa sekta hizo za afya utaratibiwa kwa uhakika ili kuweza kuijenga
jamii salama.
Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la
Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la
kusimamia na kuratibu shughui za Afya moja nchini.
MWISHO.
Post A Comment: