Wednesday, 1 May 2019

RC SHIGELLA AWAPIGA MARUFUKU TABIA YA WAKUU WA WILAYA ZA MKOA HUO KUWAWEKA NDANI WAFANYAKAZI

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) happines Sima akizungumza wakati wa maadhimisho hayo leo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akikabidhi zawadi ya TV kwa wafanyakazi mbalimbali
Sehemu ya watumishi wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa Martine Shigella
 Sehemu ya wafanyakazi na wananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo leo
Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kushoto ni Meneja wa Mfuko huo mkoa wa Tanga Happines Sima akiweka sawa mwamvuli wakipita mbele ya mgeni rasmi


MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amewapiga marufuku wakuu wa wilaya za mkoa huo kukamatwa kwa watumishi na kuwekwa ndani wafanyakazi kwa misingi isiyofuata sheria na taratibu zilizopo nchini.

Shigella aliyasema hayo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambapo kimkoa iliadhimishwa kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga ambapo alisema kama sio kosa ambalo linaweza kuhatarisha amani, linalohusisha na wizi, mauaji.

Alisema badala yake watumie taratibu za kisheria wawafikisha kwenye mamlaka za waajiri wao waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu sheria zilizopo ili kuweza kuwarekebisha kitabia.

“Mfanyakazi anaweza akawa amechelewa lakini anaweza kuwa na sababu za msingi lakini haumsikilizi wala haufanyi hivyo unamuaaguza Mkuu wa wilaya (ODC) amkamate amweke ndani hii sio sawa acheni kutumia madaraka yenu vibaya”Alisema

Alisema wakifanya hivyo watakuwa wamejenga misingi ya utawala bora, haki za binadamu ikiwemo utamaduni na utaratribu wa kuheshimia jambo ambalo litasaidia kuwawezesha kupiga hatua ya kubwa za kimaendeleo kwao na jamii zinazowazunguka.

“RPC wafikishie wakuu wa Polisi wilaya za mkoa huu kwamba kuanzia sasa wa wafanyakazi kwenye mkoa wa Tanga kama sio la kuhatarisha amani,wizi ,mauaji ni marufuku kuwekwa ndani wafanyakazi kwa misingi isiyofuata taratibu “Alisema .

Hata hivyo aliwataka lazima waweze kuweka mazingira mazuri ya kuwajenga wafanyakazi wao ili waweze kuona kosa walilofanya waweze kujutia na kuweza kujirekebisha badala ya kutumia mamlaka waliyonayo vibaya.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment