Thursday, 2 May 2019

RC MAKONDA aifagilia Manispaa ya Ilala kuwa wa kwanza Kitaifa mapato
Na Heri Shaaban

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda , ameipongeza Manispaa ya Ilala kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa ,katika ukusanyaji wa Mapato ya Serikali.

Makonda alitoa pongezi hizo kwa Watendaji wa Ilala  Dar es Salaam jana,wakati wa kikao cha Majumuisho ya ziara yake Mkoa wa Dar es Salaam wakati alipokuwa akiongea na Watendaji wa manispaa zote.

"Nimefarijika sana katika Mkoa wangu Manispaa ya Ilala imevuka lengo la ukusanyaji mapato robo ya mwaka  wamefikia  asilimia 78  naziomba halmashauri zingine muongeze juhudi  mkoa wetu ufanye vizuri zaidi " alisema Makonda

 Aliwataka Manispaa ya Ilala kuendelea katika ukusanyaji wa fedha za serikali speed hiyo isirudi nyuma

Alimwagia sifa *wakurugenzi* wa Halmashauri na watendaji kwa *kusimamia vizuri ukusanyaji wa Mapato* jambo lililopelekea *Dar es salaam kuibuka namba moja kitaifa* katika Makusanyo ya mapato katika *Robo ya Mwaka.


Alisema mpaka sasa wamefanikiwa  kukusanya kiasi cha silingi *Bilioni 118.4* ukifuatiwa na Mkoa wa Dodoma uliokusanya Shilingi Bilioni 57.3, wilaya  iliyoongoza Kitaifa Ilala ikifuatiwa na
Kinondoni pamoja na Temeke iliyoshika nafasi ya Tatu kitaifa.

Aidha  Makonda amewahimiza Watendaji kuendelea kusimamia  vyema makusanyo ya kodi pasipo kuwabugudhi wananchi ili kuwezesha Mkoa huo kuendelea kushika namba moja.

Wakati huo huo Makonda alimwagia sifa Wilaya ya Ilala kwa kufanya vizuri katika utoaji wa mikopo vikundi vya halmashauri ya Ilala hadi Wajane  wamepata.

Katika hatua nyingine aliwagiza Wakuu wa Wilaya kuweka mkakati wa kuorodhesha viwanda vyote vipya ambayo vipo katika wilaya yao.
Mwisho
Arnatogluo Dar es Salaam April 30/2019

No comments:

Post a comment