Tuesday, 14 May 2019

Nandy afunguka mipango ya ndoa na Ruge ilivyokuwaMsanii wa muziki Bongo, Nandy ameweka wazi kuwa walipanga kufunga ndoa Machi mwaka huu na aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group (CMG), Ruge Mutahaba.

Ikiwa ni takribani miezi mitatu sasa tangu tasnia ya habari impoteze mmoja wa wadau wa kubwa, Ruge Mutahaba, aliyekuwa mpenzi wake, mwanamuziki amemkumbuka kwa namna yake akieleza jinsi kifo  kilivyozima  ndoto zao.

Nandy ameeleza hayo wakati akihojiwa na Ayo Tv na kudai kuwa uhusiano wao ulikuwa wa siri kwa kuwa walikubaliana kulifanya suala hilo kuwa binafsi mpaka watakapokamilisha taratibu zote.

Amesema kuwa mara kadhaa alikuwa akikanusha kuhusu uhusiano huo kwa kuwa waliona hakuna haja ya kuweka wazi.

“Hatukupenda uhusiano wetu uendeshwe na mitandao, tulikuwa tunajaribu kutengeneza njia ya maisha yetu binafsi ili kufikia lengo letu. Hatukutaka life style  (mtindo wa maisha) ya mahusiano ya awali ya Ruge yajitokeze kwenye maisha yetu,”

Itakumbukwa kuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ltd. Ruge Mutahaba alifariki Dunia february 26 mwaka huu nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu.

No comments:

Post a comment