Friday, 17 May 2019

Mbio za John Akhwari Kufanyika June 9 Mwaka huuNa Ferdinand Shayo,Arusha.
Mbio za mwanariadha mkongwe maarufu kama John Akhwari zinatarajia kufanyika June 9 katika jiji la Arusha na kuhudhuriwa na wanariadha wa kitaiafa na kimataifa ambao watafika kuchuna  vikali katika mbio hizo za kilomita 21 na 5 na 2.
Muandaaji wa  mbio hizo Sylvester Urau amesema kuwa tayari wanariadha kutoka nje ya nchi wamethibitisha kushiriki katika mbio hizo huku mwanariadha mkubwa wa kitaifa Alphonce Felix Simbu amethibitisha kushiriki katika mbio hizo za kimatiafa.
Muasisi wa Mbio hizo John Stephen  Akhwari amesema kuwa mbio hizo zinalenga kuwahamasisha vijana kushiriki katika mbio za kimataifa na kuleta medali za ushindi nchini ili kuleta chachu katika tasnia ya mchezo wa riadha miongoni mwa vijana.
Mwenyekiti wa Chama cha Riadha mkoa wa Arusha Jackson Busiru  amesema kuwa tayari maandalizi yamefanyika kwa njia zitakazotumika katika mbio hizo ambazo zinalenga kuenzi mchango wa mwanariadha john Akhwari  katika michezo ya kimataifa.
John Stephen Akwar alijizolea umaarufu  katika mbio za kimataifa za Mexico city Games  mwaka 1968  ambapo nukuu yake maarufu inasema “Nchi yangu haikunituma nianze mbio bali ilinituma kumaliza mbio”

No comments:

Post a comment