Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya
Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari,
akisindikizwa kuingia ukumbini na mmoja wa viongozi wa CCM.
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari, akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Cholaje Mohamed.
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari, akipa kiapo cha uaminifu kwa chama pamoja na viongozi wa CCM
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari, akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Cholaje Mohamed.
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari, akipa kiapo cha uaminifu kwa chama pamoja na viongozi wa CCM
Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuiya ya Wazazi
Taifa, Cholaje Mohamed, akizungumza na wana CCM baada ya kukabidhi kadi kwa
aliyekuwa Katibu wa CUF Makurumla, Shomari Chahasi.
|
NA MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA Katibu Kata wa Chama cha Wananchi (CUF) kata ya
Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari amekihama
chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Chahasi amerudisha kadi ya CUF na kukabidhiwa ya CCM leo na
Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Cholaje Mohamed
katika mafunzo ya viongozi wa jumuiya hiyo ngazi ya kata.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi hiyo, Chahasi amesema
amefanya uamuzi wa kuhamia CCM kutokana na haki walizokuwa wakizipigania akiwa
CUF kuanza kutekelezwa na Rais Dk. John Magufuli pamoja na mshikamano uliopo
ndani ya chama hicho tawala.
Amesema Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba amekuwa
akipigania haki za kiuchumi hasa kwa wafanya biashara wadogo ambapo sasa
wametambulika na serikali.
“Kwa sasa machinga tumeanza kupata neema ya kutekeleza
shughuli zetu bila kubughudhiwa na sasa tumepatiwa vitambulisho vya kutambua
shughuli zetu,” amesema Chahasi.
Ameongeza kuwa Mungu amemteua Rais Magufuli kuwakomboa wanyonge
hivyo Watanzania hawana budi kumuunga mkono.
Aidha aliwataka kundi alilokuwa anafanya nalo kazi maarufu
kama Mungiki kumuunga mkono uamuzi wake kwa kuwa siasa zinabadilika na kila
mmoja anahitaji maisha bora, uchumi na maendeleo kwa Taifa.
Kwa upande wake Cholaje amesema wanaamini Chahasi atakuwa
na msaada mkubwa katika CCM kwa kuwa ataonesha mapungufu waliyonayo vyama vya
upinzani kwa kusaidia kuyaeleza kwa wananchi.
“Ni siku ya neema kwa ngazi zote za chama kuanzia tawi hadi
taifa kwa kuwa tumemchukua mpiganaji wa CUF ambaye alikuwa msaada mkubwa kwa
Lipumba,” amesema Cholaje.
Aliongeza kuwa wanatarajia Chahasi atakuwa sehemu ya
Kampeni kuanzia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Chahasi amekuwa mwanachama wa CUF tangu mwaka 1999 na
anatajwa kuwa alikuwa ni sehemu ya wanamkakati wa waliofanikisha ushindi wa
udiwani wa sasa kupitia CUF katika Kata ya Makurumla, Omari Kombo ‘Kijiko’.
Mwisho
Post A Comment: