Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Daudi Mafwimbo akizungumza leo wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari Duniani ambapo kwa mkoa wa Tanga ilifanyika ukumbi wa Regal Naivera kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (UTPC) Hassani Hashim anayefuatia ni Makamu Mwenyekiti wa UTPC Lulu George
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (UTPC) Hassani Hashim akizungumza wakati wa maadhimisho hayo kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Daudi Mafwimbo kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa UTPC Lulu George
Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani hapa Alex Abraham akiwasilisha taarifa kwenye maadhimisho hayo


Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (UTPC) Hassani Hashim kulia akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa UTPC Tanga Lulu George


AFISA Uhisiano wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Waandishi wa Habari kushoto ni Amina Omari kutoka Gazeti la Mtanzania na Raisa Saidi wa gazeti la Mwananchi wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa maadhimisho hayo
Kamishna wa NCCR Mageuzi Mkoani Tanga Ramadhani Manyeko kulia akiwa na Mwandishi Mwandamizi wa gazeti la Citizen mkoani Tanga George Sembony kwenye maadhimisho hayo
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga Lupaksyo Kapange akiwa kwenye maadhimisho hayo
Sehemu ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali mkoani Tanga wakifuatilia maadhimisho hayo
NA MWANDISHI WETU, TANGA.

WAANDISHI wa Habari mkoani Tanga wametakiwa kutumia vema kalamu zao katika kuhabarisha umma kwani wakiitumia vibaya kwa kutokuzingatia maadili inaweza kuibomoa jamii na kuleta madhara.

Hayo yalisemwa leo na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Daudi Mafwimbo wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari Duniani ambapo kwa mkoa wa Tanga ilifanyika ukumbi wa Regal Naivera.

Alisema kama waandishi wa habari wakishindwa kuzingatia suala hilo licha ya kuibomoa jamii lakini pia inaweza kuleta madhara yanayoweza kuwa histoiria kwa jamii zinazowazunguka

“Ndugu zangu leo hii tunaadhimisha siku ya Uhuru wa vyombo vya habari lazima tuzingatie miiko na maadili yenu kwa lengo usalama na mustakabali wa jamii kwani muandishi wa habari bila jamii sawa na samaki bila maji wanategemeana lakini kubwa tujikite kurudi kukumbuka miiko ya uandishi wa habari “Alisema Kaimu RPC

“Lakini pia wakati tunaadhimisha siku hii muhimu leo kwa waandishi wa habari na wadau wa habari tuwakumbuke ndugu zetu wana habari na wana jamii waliopoteza uhai wao kwa lengo la kuhakikisha jamii inapata habari au kuelimishwa”Alisema

Hata hivyo aliwataka kuhakikisha wanajikita kwenye kuandika habari ambazo zitakuwa zitachochea ukuaji wa maendeleo kwa jamii ikiwemo kuibua changamoto zilizopo.

Awali akiwasilisha Taarifa ya Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (TPC) Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani hapa Alex Abraham alisema wamekuwa na mahusiano mazuri na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) ambao wamekuwa wakiwapa mafunzo mbalimbali ya kitaaluma kwa wanachama chini ya udhamini wa SIDA.

Alisema siku ya leo waandisi na tasnia ya habari kwa ujumla huitumia kwa kuwakumbuka na kuwapa heshima waandishi ambao wamepata matatizo mbalimbali wakiwa kazini na hata wengine kufikia hatua ya kupoteza maisha.

“Kwa uhuru wa kujieleza ni haki ya msingi na muhimu kuweza kufikia haki nyenginezo ambazo zimo katika matamko mbalimbali ya kimataifa ya haki za binadamu, miaka miwili baadaye baada ya azimio la Windhoek yaani mwaka 1993 Baraza la Umoja wa Mataifa (United Nations General Assembly) likaitambua rasmi na kuitangaza Mei 3 kuwa siku ya Uhuru wa Habari Duniani “Alisema

Kauli mbiu ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani inasema “Jukumu la UTPC na klabu za waandishi wa habari kuchangia uchaguzi huru na haki”
Share To:

Post A Comment: