Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amesema hamna serikali ambayo imeendelea bila maendeleo ya vitu, hivyo miradi mikubwa ambayo serikali imekuwa ikitekeleza ni kwa nia nzuri.

Amebainisha hayo leo asubuhi wakati akihojiwa na East Africa Radio ambapo amegusiana na madai kuwa fedha imepotea mtaani na tuhuma za watu kutekwa.

"Kwanza ukisema huna pesa mfukoni, lazima useme hiyo pesa imechukuliwa na nani. Unaposema kuwa biashara 16,000 zimefungwa wakati huo kuna biashara zaidi ya laki moja zimefunguliwa"," ameeleza.

Kuhusu madai ya watu kutekwa, hilo amesema kuwa, "Suala la watu kutekwa au kupotea watu, kwa nchi zinazoendelea huwa linatokea. Serikali hatuwezi kujua mahusiano ya watu wote, ila inachofanya serikali ni kulinda usalama wa raia, huwezi kusema kuwa suala la utekaji limeanza awamu ya tano"
Share To:

msumbanews

Post A Comment: