Wakurugenzi 10 wa Halmashauri za Wilaya wametakiwa Kuhakikisha kuwa mradi wa timiza ndoto zako kwa wasichana wenye Balehe waliopo mashuleni na walio nje ya mfumo wa elimu unatekelezwa kama ilivyopangwa na Serikali ili kuleta matokeo chanya.

Akizungumza kwaniaba ya Waziri wa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama Mei 25, 2019 Wilayani Bahi Dodoma wakati wa uzinduzi wa mradi huo,  Katibu Mkuu Wizara hiyo Dorothy Mwaluko amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuona mradi huo unaleta ukombozi wa kweli kwa motto wa kike.

“Waliopo shuleni na nje ya mfumo wa elimu ni vyema mkatambua kuwa mradi huu ni fursa ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuepuka vishawishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwani Serikali inatambua kuwa kumuwezesha motto wa kike ni kuiwezesha jamii nzima” Alisema Doorthy.

Mradi huu unatekelezwa katika mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida ambapo jumla ya Halmashuri 10 katika mikoa hiyo zinanufaika.

Utekelezaji wake unatokana na usaidizi wa fedha kutoka Mfuko wa Dunia kwaajili ya kuendeleza mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na athari zake.

Akifafanua amesema kuwa watekelezaji wa mradi huo wanalo jukumu la kuwajengea uwezo wanufaika ili hata baada ya kipindi cha mradi waweze kujitegemea na kuondokana na utegemezi kutoka kwa serikali ambapo kwa sasa wanafunzi kutoka Kaya masikini wanawezeshwa kupata taulo za kujisitiri pamoja na mahitaji mengine ikiwemo sare za shule.

Aliongeza kuwa wanafunzi wote wanapaswa kutambua kuwa Serikali inawekeza fedha nyingi katika mradi huo kwa kutambua umuhimu wa kundi hilo ili kujikwamua kielimu na kutumia vyema vipaji walivyonavyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi  Mwanamisi Mukunda akizungumza kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge amasema kuwa mradi huo umesaidia kuongeza kiwango cha ufaulu katika Wilayahiyo, mahudhurio ya wanafunzi shuleni yameongezeka kwa kiwango kikubwa.

“Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutuletea mradi huu katika Wilaya yetu kwani umeonesha mafanikio makubwa kwa kipindi cha majaribio ambacho umetekelezwa kwani umewanufaisha Wanawake Vijana wenye umri wa kati ya miaka 10- 24”, alisisitiza Mwanahamisi.

Akifafanua amesema kuwa mradi huo umefikia Kaya 265 na wasichana 129 unawanufaisha wasichana balehe waliopo shuleni na wale wa nje ya shule  45.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko amesema mradi huo ni wa miaka 3 na unatekelezwa katika mikoa 3 ambapowanufaikawamradiwalionjeyashulewatajengwewauwezokwakupewastadizamaisha.

Alitaja sababu za kuwalenga wasichana wanaobalehe Dkt. Maboko amesema kuwa ni pamoja na kundi hilo kuwa waathirika wakubwa ambapo asilimia 80 yamaambukizi ya VVU yamewaathiri vijana wa kundi hilo.

Mmoja wa wazazi wa wanafunzi walionufaika na mradihuo Mayasa Mussa amesema kuwa wanafunzi wanafurahia mradi huo na ari ya kwenda shule imeongezeka kwani kila mwezi wanapokea elfu 25,000/- kwa mwezi kuwawezesha kukidhi mahitaji muhimu ya wanafunzi hao ikiwemo kupata tauloza kike, sare za shule na mahitaji mengine.

Mradi wa Timiza ndoto zako unatekelezwa katika mikoa 3 na Halmashuri 10 ukilenga kuwawezesha wasichana waliobalehe wakiwa mashuleni na wale walio nje ya mfumo wa elimu.
Share To:

Post A Comment: