Mchezaji wa timu ya Simba SC, Hassan Dilunga amewaomba radhi viongozi na mashabiki wa JKT Tanzania baada ya kuwafunga jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Timu ya Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 likifungwa na Dilunga mnamo dakika ya mwisho kabisa ya mchezo na kuifanya Simba ipate alama tatu muhimu.

Baada ya mchezo Dilunga aliibuka na kusema anawaomba radhi JKT kwani aliwahi kuichezea timu hiyo na aliondoka bila ugomvi.

Dilunga ameeleza kuwa kwa sasa wako kwenye harakati za kuchukua ubingwa wa pili mfululizo hivyo hakuwa na namna ya kufunga.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: