Mwezeshaji wa Mafunzo ya kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama, kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Profesa, Rudovick Kazwala, akifundisha kwa vitendo namna ya kutumia Vifaa vya kitaalam vya Kinga Binafsi, wakati wa mafunzo hayo kwa wataalamu wa sekta za Afya  kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.

Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya  kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya kwa Halmashauri zilizopo mipakani wakiwa wamevaa vifaa vya Kitaalamu vya Kinga Binafsi, wakati wa  Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.


 Mratibu wa Kitaifa, Dawati la Afya moja, lililopo Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka, akisisitiza  umuhimu wa sekta za Afya kushirikiana wakati wa mafunzo ya kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama kwa wataalamu wa sekta za Afya  kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe
 Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini, Dkt. Hezron Nonga akisisitiza  umuhimu wa kutumia Dhana ya Afya moja wakati wa mafunzo ya kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama kwa wataalamu wa sekta za Afya  kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe
 Mwezeshaji wa Mafunzo ya kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama, kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, Niwael Mtui,  akifundisha namna ya kudhibiti magonjwa ambukizi maeneo ya mipakani wakati wa mafunzo hayo kwa wataalamu wa sekta za Afya  kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.
 Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya  kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, wakiwa katika makundi ya majadiliano wakati wa mafunzo ya Kuimarisha Udhibiti wa magonjwa ambukizi kwa kutumia Dhana ya Afya moja kwa maeneo ya mipakani, Mafunzo  hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.

Mwezeshaji wa Mafunzo ya kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama, kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Emmanuel Swai, akifundisha namna ya kudhibiti magonjwa ambukizi maeneo ya mipakani, wakati wa mafunzo hayo kwa wataalamu wa sekta za Afya  kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.


Dhana ya Afya moja ambayo hujikita katika kujumuisha sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu imeendelea kufundishwa kwa Wataalamu wa sekta hizo za Afya, ikiwa ni Sekta ya Afya  ya Binadamu, Wanyamapori, Mifugo, Kilimo na Mazingira, ili wataalamu hao watumie dhana hiyo kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama  ambayo hutokea mara kwa mara katika maeneo ya mipakani kutokana na kuwepo kwa  mwingiliano mkubwa kati ya  watu na wanyama katika mazingira yao.

Pamoja na Mwingiliano huo wenye faida kubwa kiuchumi lakini pia unasababisha kuenea kwa vimelea   kwa uharaka zaidi na kusababisha magonjwa kwa binadamu, wanyama na mimea katika mazingira yao, hivyo ili kuimarisha Afya ya binadamu, Shirika la Chakula na Kilimo  la Umoja wa Mataifa (FAO), pamoja  na watalaamu kutoka Wizara ya Mifugo na  Uvuvi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine wamewapa mafunzo wataalamu wa sekta za Afya wanao toka katika Halmashauri za Mkoa wa Mbeya na Songwe zilizo mipakani juu ya namna ya kujiandaa na kukabili magonjwa ambukizi kama  vile Ugonjwa wa Kimeta kwa kutumia Dhana ya Afya  moja.

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia tarehe 29 Aprili hadi,tarehe 3 Mei, 2019, Mkoani Songwe, Mkurugenzi wa Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, ambaye aliwakilishwa na Mratibu Kitaifa, Dawati la Kuratibu Afya Moja, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka,  alibainisha kuwa ushirikiano wa wataalam na sekta za Afya  kwa kutumia dhana ya Afya Moja hivi sasa ni agenda ya dunia nzima. Aidha, alieleza kuwa Dhana hiyo imekusudiwa kutumika maeneo ya mipakani   ambapo mwingiliano huo huchochewa na wasafiri kutoka eneo moja kwenda jingine, ongezeko la watu duniani, mabadiliko ya tabia nchi,  utandawazi, ongezeko la mahitaji ya maji na chakula.

Awali akiongea katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini, Dkt. Hezron Nonga alibainisha kuwa  sekta za Afya zikishirikiana katika Kudhibiti magojwa zitasaidia kuimarisha Afya ya Binadamu kwa kuwa kila sekta itakuwa inachukuwa tahadhri kwa wakati. Aidha alibainisha kuwa  vimelea vingi vinavyo sabababisha magonjwa kwa binadamu asilimia (60%) vinatoka  kwa wanyama pori na mifugo na maambukizi yanatokea pale binadamu anapoingilia maskani ya wanyama hao bila tahadhari, hivyo Afya moja ikitumika maeneo ya mipakani itasaidia kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi yanayotokana na shughuli za mwingiliano wa wanyama na binadamu zinazofanyika sana maeneo ya mipakani.

Katika kuhakikisha watalaam hao kutoka sekta za Afya wanaweza kutumia Dhana  hiyo katika kudhibiti magonjwa katika maeneo ya mipakani wameweza kujengewa uwezo wa namna ya kutoa taarifa za milipuko ya magonjwa ambukizi kama vile ugonjwa wa Kimeta, pindi unapotokea maeneo ya mipakani, Namna ya kuunda vikosi vya kufuatilia na kukabili Ugonjwa, Mawasiliano wakati wa kufuatilia na kukabili magonjwa hayo kwa kutumia Dhana ya Afya moja,  pamoja na masuala ya kutumia vifaa Kinga Binafsi vya Kitaalamu.

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za Afya moja nchini. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja  kwa kushirikiana Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) waliandaa na kuratibu mafuzo hay
Share To:

Post A Comment: