Mratibu wa Masoko kampuni ya Harsho Group inayozalisha mifuko mbadala,Caroline Satsif akionyesha wateja waliotembelea katika banda hilo. 
Mmoja wa mtendakazi katika kampuni hiyo akionyesha aina ya mifuko ambayo ni rafiki kwa mazingira wataanza kuisambaza kwa wananchi kwa bei nafuu.

Na Vero Ignatus, Kilimanjaro
Wazalishaji wa mifuko mbadala wametakiwa kuchangamkia fursa kuzalisha mifuko kwa wongi ya kukidhi mahitaji ambayo ni rafiki wa mazingira kwani tayari mkoa wa Kilimanjaro umeshapiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki. 
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira alipotembelea maonyesho ya wiki ya elimu katika uwanja wa Mashujaa Wilayani Moshi ,amesema kuwa wajasiriamali wanaotumia vifungashio vya mifuko ya plastiki wanapaswa kujiianda mpaka muda uliopangwa na serikali Mwezi June mwaka huu waweze kuondokana na matumizi ya plastiki.
Kwa sasa mkoa wa Kilimajaro ni marufuku kutumia mifuko ya plastiki tumeanza mapema ili watu wajiandae ikifika mwezi wa sita mwaka huu watu wawe kwenye mstari na kuzoea kutumia mifuko mbadala tunashukuru wenzetu wa Harsho Group wameanza kuzalisha mifuko ya kutosha ” Alisema Dkt.Anna
Nae Mratibu wa Masoko kampuni ya Harsho Group inayozalisha mifuko mbadala,Caroline Satsif  alisema kwa mkoa wa Kilimanjaro wamejianda vyema kuzalisha mifuko ambayo ni rafiki kwa mazingira na kuisambaza kwa bei nafuu.
Caroline alisema kuwa wanazalisha mifuko laki 5 kwa siku ambayo inatosheleza mahitaji ya mkoa wa Kilimanjaro na mikoa jirani pamoja na Tanzania nzima hivyo wamejiandaa kuzi ba pengo la mifuko ya plastiki.
Anaeleza kuwa mifuko hiyo inaweza kufuliwa zaidi ya mara tano na iwapo ikitupwa inaweza kuoza na kuwa mbolea katika ardhi.
Mkazi wa Manispaa ya Moshi Roman Mnzava alisema kuwa hatua ya Mkoa wa Killimanjaro kupiga marufuku matumizi ya plastiki utasaidia kuokoa mazingira na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ambao ni kitovu cha utalii mkoani hapa
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: