Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,  Jerry Cornel Muro, Amesema watu wote watakaotuhumiwa ama kujihusisha na vitendo vya ubakaji na kuwapachika mimba watoto wilayani humo watakiona cha mtema kuni kuwa hawatapata dhamana pindi wakikamatwa na kufikishwa polisi

DC Muro Ametoa kauli hiyo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha katika maadhimisho ya miaka 20 Ya shirika la kimataifa  la Compasion International la kuhudumia watoto waishia katika mazingira magumu.

Muro ameeleza kuwa tangu alipoingia wilayani hapo alikutana vitendo vya ubakaji na mimba kwa wanafunzi vikiripotiwa 80 kwa mwaka uliopita lakini juhudi hizi za kuwakamata watuhumiwa zimesaidia kupunguza vitendo hivyo hadi vinne kwa miezi nane iliyopita

Kwa upande wa Viongozi wa Shirika hilo pamoja na viongozi wa Dini wanasema juhudi wa kuwalinda watoto zinahitajika, ambapo katika kutekeleza hilo wamekuwa wakiwahudumia watoto takribani 6000 kwa mkoa wa Arusha pekee ili wafikie ndoto zao.

Katika maadhimisho hayo, Compasion Internatinal Imetoa Mashine tatu za kupima Presha, na  Mashuka 200 kwaajili ya hospitali wilayani Arumeru kwenye Wodi za watoto.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: