Thursday, 11 April 2019

WAKAZI WA KIMARA BONYOKWA WAPATIWA MAJISAFI NA SALAMA

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) (aliyenyanyua mikono) akifurahia mara baada ya kutobolewa bomba la maji litakalokuwa likiwasambazia wakazi wa Bonyokwa na Vitongoji vyake. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) akiangalia mafundi wakiendelea na kazi ya kuunganisha bomba.
Moja ya bomba lililofungwa kwa wakazi wa Bonyokwa kuendelea kupata maji. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Wakazi wa Kimara Bonyokwa na vitongoji vyake wameanza kufurahia huduma ya majisafi na majitaka kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA). Wakizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam wakazi hao wamefurahia huduma hiyo baada ya kuunganishiwa maji baada ya kukaa kipindi kirefu wakitumia maji ya Kisima. Mmoja ya wakazi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mama K amesema kuwa ni neema ya ajabu kwa wao kupata maji maana hawakutarajia kama wataweza pata huduma hiyo. "Ni jambo la Kumshukuru Mungu sisi wakazi wa Bonyokwa kupata maji maana tumekuwa tukiyaota kwa muda mrefu bila mafanikio," amesema Mama K. Upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja ameshukuru wakazi hao kwa uvumilivu wao na kuendelea kuwaamini ili waweze kuwapatia huduma. Mhandisi Luhemeja amesema kuwa DAWASA imejipanga kuendelea kutoa maunganisho kwa wakazi wa pembezoni mwa mji na ifikapo 2020 zoezi litakuwa limekamilika. -- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 *www.kajunason.com * *"Everything is Possible Through Peace & Stability''*

No comments:

Post a comment