NA Imma Msumba
Jamii kuanzia ngazi ya familia zimetakiwa kuendelea kuwajengea uwezo wasichana ikiwa ni Sehemu ya kuwaelimisha Masuala mbalimbali yanayo husiana na afya ya uzazi Kutoka na asilimia kubwa ya wasichana na Vijana kutokuwa na uelewa juu ya Afya ya uzazi katika maisha ya kila siku.

Ili kumjengea uwezo kwa kumuelimisha,kujitambua na kuchukua tahadhari kutokana na vihatarishi katika mazingira wanayo ishi Vijana hao Taasisi ya kimataifa ya "Chanya Change" imeendelea kutoa elimu kwa wasichana zaidi ya 100 Kutoka shule mbalimbali Jijini Arusha Lengo likiwa ni kuwasaidia kujitambua,kutoa hamasa katika masomo ya Sayansi na kupata mafunzo ya tehama kwa maslahi ya vizazi vya Sasa na baadae.

Akizungumza na Msumbanews muandaaji wa warsha hiyo iliyo andaliwa na taasisi ya Kimataifa ya "+Chanya Change" kwa ajili ya wasichana Bi Pamela Chogo amesema Msichana ananafasi kubwa katika kuchochea shughuli za kimaendeleo ya taifa hususani katika Masuala ya Sayansi na teknolojia (TEHAMA) kwani Wanawake wengi wamekuwa wakutumia changamoto hiyo Kuwa fursa katika jamii wanazo ishi hatimae wameleta chachu ya Maendeleo kuelekea Tanzania ya Viwanda.

"Ni wakati muafaka kwa jamii kuondokana na mtazamo Hasi kuhusu mtoto wa kike Kuwa hawezi kufanikisha Mambo muhimu katika jamii,mwanamke ndio msingi wa maendeleo"alisema Pamela.

Amesema bado kumekuwa na ombwe kubwa kwa baadhi ya wasichana kuto jitambua kutokana na kukosa elimu ya Afya ya uzazi kwa Vijana ngazi ya familia hivyo wazazi wanajukumu kubwa la kuelimisha Watoto wao wa kike wakaribiapo Rika la balehe ili kuepukana na ongozeko la ndoa,mimba za utotoni.

"Wazazi wengi bado wanatamaduni za kizamani ambazo zimekuwa chanzo Cha wasichana wengi kujiingiza Kwenye makundi Hasi yanayo pelekea kupata magonjwa na Matumizi ya madawa ya kulevya kwa kukosa elimu ya jinsi"

Anna Mahenge ni mtaalamu wa Masuala ya Afya ya uzazi anasema familia nyingi zimekuwa zikishindwa kukaa na mabinti zao na kuwaeleza ukweli kuhusu afya uzazi suala ambalo limekuwa likichangia ongezelo la vihatarishi na maambukiIi ya magonjwa ya zinaa pamoja na mimba za utotoni.

"Kuficha ficha mambo kwa wazazi juu ya wasichana kuhusu maumbile na maungo ya uzazi bado ni Changamoto kwa jamii, hivyo jamii ibadilike"alisema muuguzi huyo.

Aidha kwa upande wao baadhi ya wasichana  washiriki katika warsha hiyo wamesema asasi za kiraia zinazo hudumia jamii waige mfano wa kinacho fanywa na taasisi ya Chanya Change ili kufika katika maeneo husika na kutoa elimu ili kukiandaa kizazi chanya kwa siku za usoni.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: