Tuesday, 30 April 2019

NAIBU MEYA IRINGA AZINDUA ALBAMU YA MSANII REHEBIAN KIGAHE IITWAYO “WEMA NA FADHILI ZA BWANA”

 Naibu meya wa manispaa Joseph Lyata ya Iringa akiwa na
msanii Rehebian Kigahe aliyekua anazindua albam inayoitwa “wema na fadhili za bwana”katika kanisa la PHM Mkwawa
Naibu meya wa manispaa Joseph Lyata Iringa akiwa viongozi wa kanisa la PHM Mkwawa wakati wa uzinduzi wa albamu ya msanii Rehebian Kigahe
 Msanii Rehebian Kigahe akiongea neno wakati wa kuzindua albamu yake ya “wema na fadhili za bwana” katika kanisa la PHM Mkwawa
Baadhi ya waumini na mashabiki wa msanii Rehebian Kigahe waliohudhulia katika uzinduzi wa albamu ya msanii huyo

 NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
NAIBU meya wa manispaa ya Iringa amewataka waumini na wananchi kote nchini kuendelea kuliombea taifa kudumisha amani na upendo uliopo ili kuepukana na machafuko kama ilivyo kwenye nchi nyingine za jirani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa album ya msanii Rehebian Kigahe inayoitwa “wema na fadhili za bwana” Naibu meya wa manispaa Joseph Lyata alisema, kupitia makanisa na madhehebu mengi kuendelea kuhubili ambani kokote kule ambako wanauwezo kuwafakia wananchi.

“Leo tunazindua album hii ya “wema na fadhili za bwana” imetuunganisha watu wote kuongea lugha moja na kuendelea kutunza amani yetu hivyo niwaombe wananchi nao waendelee kuhubili amani” alisema Lyata

Lyata alimpongea msanii aitwaye Rehebian Kigahe kwa kuandaa albam ambayo imebeba ujumbe wa kumuabudu na kumsifu mwenyezi mungu jambo linalopelekea watanzania nao kuiga mfano wa msanii huyu kusisitiza amani iliyopo

“Naomba kwa dhati  yangu kumpongeza msanii huyu kwa kazi nzuri ya kumpongeza msanii huyu kwa kutunga nyimbo za kumwabudu mwenyezi mungu kwa kuwa ujumbe wake utaenea nchi nzima kwa kutumia nyimbo zake”alisema Lyata

Aidha Lyata aliwaomba watanzania kuinunua albu ya msanii Rehebian Kigahe kwa kuwa imejaa nyimbo za kumsifu bwana na zenye mafunzo mengi kwa jamii huku lengo likiwa kuwasaidia na kuwainua wasanii kama Rehebian Kigahe ambao bado hawajajulikana hivyo.

“Albam hii mimi nimeipenda na nimesikiliza nyimbo zake zinaujumbe mzuri sana,ningependa kila mtanzania aipate albam hii kwa kuwa ujumbe wake unatufanya tuendelee kumwabudu mwenyezi mungu” alisema Lyata

Kwa upande wake msanii wa nyimbo hizo za injili Rehebian Kigahe alimshukuru Naibu meya wa manispaa ya Iringa kwa ujumbe wake kwa taifa juu ya albam yake na kuwaomba watanzania wamuunge mkono ili aweze kuwahubilia wananchi kwa kutumia uimbaji.

Namshukuru mungu leo nimezindua albam yangu ambayo inanyimbo tisa na albam hii inaitwa “wema na fadhili za bwana” ambayo nauhakika wa kuwa atakayesikiza albam hii atapata wokovu mzuri kwa ujumbe ambao nimeukalisha kwa njia ya nyimbo hizi” alisema Kigahe

Kigahe aliwaomba watanzania kuitafuta na kuinunua albamu hiyo ya “wema na fadhili za bwana” kwa kuwa inamafunzo mengi sana yaliyopo ndani ya nyimbo zilizopo humo ndani

No comments:

Post a Comment