Monday, 29 April 2019

Mbunge ameiomba serikali ieleze chanzo cha upungufu wa nguvu za kiume.Mbunge wa Ulanga kwa tiketia ya CCM, Goodluck Mlinga ameiomba serikali ieleze nini chanzo cha upungufu wa nguvu za kiume.

Mbunge huyo akiuliza swali la nyongeza leo Bungeni, pia amezitaja baadhi ya dawa za kuongeza nguvu za kiume.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi kwa niaba ya waziri wa Afya amesema tatizo la nguvu za kiume linatokana na sababu mbalimbali.

"Kwa sababu zinazopokea kupungua kwa nguvu za kiume ni nyingi, ikiwepo magonjwa mbalimbali kama vile kisukari na msongo wa mawazo," ameeleza.

Awali Waziri huyo alieleza, "Kumekuwa na taarifa nyingi za dawa zinazoweza kukuza maumbile, wale ambao wanatoa taarifa hizi bila ya uthibitisho wanatakiwa wachukuliwe hatua, mpaka sasa hakuna dawa yoyote ambayo kitaalamu imethibitishwa na imepewa kibali kwa ajili ya matumizi kama hayo".

No comments:

Post a Comment