Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kambi ya macho kwenye shule ya Sekondari Maawal Jijini Tanga chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanzania wakishirikiana na Mbunge huyo chini ya Ufadhili wa  better Charity ya nchini Uingereza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Mwenyekiti wa Bilal Muslim Africa Mohsin Abdallah (Shein)

 Mwenyekiti wa Bilal Muslim Africa Mohsin Abdallah (Shein) akizungumza wakati wa uzinduzi huo kulia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto ni Mkuu wa Maawal Sheikh Mohamed Hariri

MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa halfa hiyo


 Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Clemence Marcel akizungumza wakati wa uzinduzi huo
 Mratibu w Bilal Muslim Mission of Tanzania Sharriff  akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo na Mratibu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania Sharrif mara baada ya kufanya uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo na mmoja wa wanafunzi ambaye alijitokeza kwenye kambi hiyo ya matibabu ya macho mara baada ya kuizindua

Sehemu ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Waziri Ummy wakati akizindua matibabu hayo
 Wananchi kutoka maeneo
 Sehemu ya wananchi wakisubiriwa kupata huduma ya matibabu wakati wa kambi hiyo
 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye kambi hiyo ya macho


MAELFU ya Wakazi wa mji wa Tanga wamejitokeza kwenye kambi ya Matibabu ya Macho inayoendelea kwenye shule ya shule ya Sekondari Maawal mjini hapa chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Mission tanzania wakishirikiana na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto chini ya Ufadhili wa  better Charity ya nchini Uingereza


Akizungumza wakati akizindua kambi hiyo ya matibabu ya Macho Waziri Ummy alisema kuwa tatizo la ugonjwa wa macho nchini limekuwa kubwa ambapo kila watanzania mia moja wanne wanakabiliwa na matatizo ya macho.

Alisema takwimu hizo zimefafanua kuwa katika idadi hiyo kila mtanzania mmoja anakabiliwa na tatizo la upofu wa mamcho na watanzania watatu wanakabiliwa na matatizo ya upungufu wa uoni wa kati na hali ya juu tatizo ambalo limekuwa kubwa sana.

Aidha alisema kwa mujibu wa takwimu wizara ya afya katika kila watanzania 100 mmoja ana tatizo la upofu huku kwa ikieleza kwa watanzania 100 kati yao watatu wana matatizo ya upungufu wa kuona wa kati na hali ya juu tatizo hilo ni kubwa kwa sababu kati ya watu 100 wa nne wana matatizo ya macho.

Kufuatia hali hiyo Waziri Ummy alitoa wito kwa watanzania kujiwekea utaratibu wa kuhudhuria kwenye vituo vya Afya ili waweze kupata matibabu pindi wanapoona kuwepo dalili za ugonjwa wa macho.

“Ukiona una tatizo la macho nenda kwenye vituo vya afya upate matibabu haraka lakini niwaambie pia wana tanga na watanzania hakikisheni mnachunguza afya ya macho na afya ya kinywa mara moja kila mwaka “Alisema

Waziri huyo aliwataka watanzania kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa hasa vyenye vitamin ikiwemo kuhakikisha wanakula mbogamboga huku akiwataka kuacha dawa kwenye macho bila kuandikiwa na daktari kwa sababu inaweza kupelekea kuharibu macho yao

Awali akizungumza katika halfa hiyo Mwenyekiti wa Bilal Muslim Afrika Mohsin Abdallah (Shein) alimshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kuhakikisha huduma za afya nchini zinaimarika kwenye maeneo mbalimbali na kuondosha changamoto zilizopokuwepo awali.

“Namshukuru Rais Magufuli miaka yote tumefanya kazi tunatumia hospitali za serikali huduma zilikuwepo lakini hazikuwa kama ilivyo sasa lakini leo serikali ya awamu ya tano hospitali zimekuwa na vifaa muhimu kwenye hospitali”Alisema

Aidha alisema wao kama bilal Muslim wamekuwa wakienda kwenye maeneo ambayo yana matukio makubwa lakini kutokana na ombi la Waziri Ummy tumeona kuja hapa kumuunga mkono pia tunashukuru mwamko umekuwa mkubwa sana,

Share To:

Post A Comment: