Ndugu John Daniel Pallangyo ameshinda kwa kishindo katika kinyanyanyiro cha kura za maoni za kuteuliwa kuwa mgombea wa kiti cha Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki  kupitia Chama cha Mapinduzi ( CCM ).

Ndugu Pallangyo ameongoza kwa kura Mia 470 kati ya kura Mia 690 na kuwashinda wagombea wenzake wake 33 ambao walijitokeza kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Arumeru.

Matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi Ndugu Humphrey Polepole yamempa ushindi John Pallangyo kwa  kura 470  huku akifuatiwa na Advocate Daniel Pallangyo aliyepata kura 50 akifuatiwa na Ndugu Sarakikya aliyepata kura 36

Baada ya kutangazwa  mshindi Ndugu Pallangyo alimuleza mwandishi wa mtandao huu kuwa 
''Nimeridhishwa na uchaguzi huu maana umefanyika kwa haki na kura zimehesabiwa bila matatizo yoyote huku ulinzi ukiwa umeimarishwa nje na ndani ya ukumbi huu Nimekuwa kwenye siasa kwa muda sasa ila namshukuru wanachama wenzangu wa wameonyesha kuwa bado wanaimani na imani hiyo imetokana na siasa safi ninazozifanya arumeru''




Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Meru wakiwa Ukumbini wakisubiri zoezi la upigaji kura kuanza.
 Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Ndugu Humphrey Polepole akihakikishia kura kwa kila mgombea.
 Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Meru akipiga kura yake ya maoni ya kumpata mwakilishi wa kiti cha ubunge kupitia chama cha Mapinduzi mapema hii leo.
 Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro akifuatiwa na Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Arusha Ndugu Sanare sambamba na Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi Taifa Ndugu Humphrey Polepole.
 Wagombea wa kiti cha ubunge kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi  wilaya ya Meru wakifuatilia matokeo ya kura za maoni kwa umakini. 

Share To:

Post A Comment: