Friday, 19 April 2019

DC Muro kuwalipa mshahara wake Wanasheria, Kisa?Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha,  Jonathan Shana amempongeza Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro kwa jitihada zake za kutatua kero mbalimbali Usiku na Mchana za wananchi wa Wilayani Arumeru.

Kamanda Shana ametoa pongezi hizo kwa Dc Muro katika ziara yake wilayani  Arumeru ambapo Pia ameshiriki kutatua kero za wananchi zinahusiana na mambo ya ulinzi ambapo amesema kuwa DC Muro amekuwa akifanya vizuri katika kutatua kero mbalimbali za wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi katika wilaya ya Arumeru.

Hata hivyo Kamanda Shana amewataka askari wa Jeshi la Polisi wanaofanya kazi kwa mazoea kuacha mara moja badala yake wafanye kazi kwa kasi aliyonayo Rais Magufuli.

Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Arumeru amemuhakikishia Kamanda huyo kuendelea kufanya kwa weledi sambamba na  shughuli za wananchi kwa kutatua kero zinazowakabili.

 DC Muro amesema amelazimika kuwatafuta wanasheria wanne kwa kuwalipa fedha katika mshahara wake kwa lengo la kuwasaidia wananchi katika utatuzi wa migogoro ya ardhi.


No comments:

Post a comment