Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizunguka kwenye uzinduzi wa Dar ya Kijani ambayo sasa imetua Wilayani Kinondoni.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, akizungumza katika uzinduzi huo.

Vijana wa CCM wakiwa kwenye uzinduzi huo Wilayani Kinondoni.

Na MWANDISHI WETU

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Rodrick Mpogolo, amewapokea wanachama wapya wa chama hicho kupitia kampeni ya Dar ya kijani inayoratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam.

Kampeni hiyo ya Dar ya Kijani ina lengo la kurudisha mitaa, kata na majimbo yote katika himaya ya chama, inawataka vijana na wanachama wote kuimarisha ushirikiano na kupata ushindi wa pamoja wenye heshima kwa chama hicho tawala.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa Wilaya ya Kinondoni, Mpogolo, amewataka vijana kuwa makini na waadilifu kwani wao ndio wataokaojenga hehima ya chama na Taifa kwa ujumla.

“Vijana ndio tunao wategemea katika uchaguzi ujao tunahitaji vijana makini na waadilifu ambao watakitumikia chama chetu cha Mapinduzi na Serikali yetu. jiepushieni mbali na tabia ambazo zitawaondelea maadili yenu. Ili mkawe viongozi makini kwani taifa letu linaitaji viongozi makini na wachapakazi .

Amesema yeye hatoita Dar ya Kijani ila anaitambua Tanzania ya Kijani kutokana na kaz kubwa inayofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi ya kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.

“Mimi sitaita Dar es Salaam ya Kijani bali nitaita Tanzania ya Kijani kwa sababu Rais wetu mpendwa Dk. John Magufuli anafanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo nchini, tunaona ujenzi wa barabara za juu pale Ubungo na tunashuhudia maendeleo makubwa yanayofanywa katika sekta ya elimu vituo vya afya, kuwasaidia wamachinga kwa kuwapa vitambulisho vya ujasiriamali, bodaboda.

“Pia ameleta usawa kwa Watanzania wote kuwa sawa. Kwahiyo kwa namna hii lazima chama chetu kiendelee kushika hatamu kwa sababu tunawatumikia wananchi ipasavyo kwa namna hii nina uhakika Tanzania inaenda kuwa ya kijani,” amesema Mpogolo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, amesema kuwa lengo la kampeni hiyo ya Dar es Salaam ya Kijani ni kuwaandaa vijana na chaguzi zijazo ikiwamo wa Serikali za Mitaa mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 ili chama hicho kipate ushindi wa kishindo.

“Lengo la Dar es salaam ya Kijani ni kuwaanda vijana wa Mkoa wa Dar es salaam katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lakini kuwataka vijana kuhakikisha wanajitokeza katika kugombea nafasi lakini pia kuhakikksha CCM kinapata ushindi wa kishindo kwa mkoa wote,” amesema Kilakala

Amesema tangu kampeni hiyo ilipozinduliwa Machi 17, mwaka huu jijini Dar es Salaam imefanikiwa kuvuna zaidi ya wanachama 500  ambao wamejiunga na chama hicho.




Share To:

Post A Comment: