Thursday, 7 March 2019

WAZIRI WA NISHATI DKT. KALEMANI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KATIKA VITUO VYA MAFUTA JIJINI ARUSHA

 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwa amefanyaziara ya kushtukiza katika kituo cha mafuta cha ORYX kilichopo clock tower jijini Arusha akiwa ameambatana na Kqmishna wa Nishati nchini, mkuu wa wilaya wa Arusha Gabriel Daqqaro na viongozi wengine waliopo katika sekta hiyo
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalimali akizungumza na Meneja wa kituo cha kuweka mafuta cha ORYX ndugu Mustapha Vrjee akitaka kujua bei za maguta wanazowauzia wateja kama ni ile iliyopangwa na serikali
 Meneja wa Kituo cha ORYX akitoa ufafanuzi kwa waziri wa Nishati kwa maswali aliyomuuliza kama wanatoaga risiti kwa wateja wao pia ametaka kufahamu huwa wanachukulia mafuta yao katika bandari ipi.
 Meneja wa ORYX Mustafa Vrjee  kama anavyoonekana katika picha mara waziri alipowasiri katika kituo hicho
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akimpa maagizo Meneja wa kituo cha ORYX Jijini Arusha jana. Picha na Vero Ignatus 
 Pichani Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha Mafuta cha PUMA kilichopo Njiro nanenane Jijini Arusha
Waziri wa nishati Medard Kalemani akimpa maagizo superviser wa kituo cha mafuata cha Puma kilichopo nanenane njiro Jijini Arusha

Na. VERO IGNATUS ARUSHA 

Waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani amefanya ziara ya kushtukiza katika vituo vitatu vya mafuta (PetroStation) kufanya ukaguzi wa kutaka kujua kama bei za mafuta ni sawa na ile iliyopangwa na serikali

Pia Waziri Kalemani alipokuwa akukagua utendaji kazi wa baadhi ya vituo vya mafuta vya mjini hapa ambapo aliagiza kuwa wafanyabiashara wote wa vituo vya mafuta kanda ya kaskazini wanatakiwa kuchulia mafuta katika bandari ya Tanga na sio Dar es Salaam na kwamba watakaokiuka agizo hilo la serikali watachukuliwa hatua.

Amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Ewura kuwaandikia barua ya onyo walewote wanaochukua mafuta katika bandari ya Dar es salamu wakati wapo Kanda ya Kaskazini

Dkt Medard alipowasili katika vituo hivyo aliweza kuzungumza moja kwa moja na wateja ambao walikuwepo wakiweka mafuta kwenye magari yao na kutaka kujua bei halali ya mafuta na kuangalia kama wamepewa risiti halali ya malipo waliyotoa

No comments:

Post a Comment