Watu watatu wilayani Muleba, mkoani Kagera  wamekutwa wakitengeneza vitambulisho bandia vinavyofanana na vile vinavyotolewa na serikali vya kuwatambua wafanyabiashara wadogo.

Pia Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Rutoro katika kata ya Ngenge, mkoani humo ni kati ya watuhumi hao.

Utakumbuka December 10, 2018, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alitoa vitambulisho 670,000 ambavyo vitagawiwa kwa wajasiriamali wadogowadogo wa mikoa yote nchini.

Ni baada ya kuona mchakato wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwapatia unachukua muda mrefu tangu alipoagiza wasajiliwe ili watambulike rasmi. Kila ambaye atapatiwa kitambulisho hicho atalipia Tsh. 20,000 ambapo atakitumia kwa mwaka mzima.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: