Tuesday, 5 March 2019

Vituo 858 vyaongezwa Uchaguzi Mkuu 2020Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage leo amezungumza na wawakilishi  wa vyama vya siasa  na kusema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  imeongeza vituo vya kupigia kura 858 kutoka 36,549 vya mwaka 2015 hadi 37,407 hiyo yote ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Jaji Kaijage ameenda mbali zaidi na kusema kuwa vituo 6,208 vimebadilishwa majina na vituo 817 vimehamishwa kutoka kijiji/mtaa mmoja kwenda mwingine.

"Vituo 19 vimeongezwa kutoka kata moja kwenda nyingine. Matokeo ya uhakiki wa vituo vya kupigia kura kwa Tanzania Zanzibar yanaonyesha vituo vimeongezeka kutoka 380 bado vituo 407," amesema Jaji Kaijage.

 Mkurugenzi wa uchaguzi wa NEC, Athuman Kihamia amezungumzia lengo la mkutano huo amesema ni kufafanua mabadiliko ya kanuni za uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura la 2008.

No comments:

Post a Comment