OFISI YA
MAKAMU WA RAIS

TAARIFA KWA
UMMA
KUHUSU UHAKIKI WA VIBALI VYOTE VYA TAKA HATARISHI
Ofisi ya Makamu wa Rais imepewa mamlaka ya
kusimamia na kuratibu masuala yote yanayohusu mazingira nchini kwa mujibu wa
Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, 2004 na Kanuni zake. Aidha, usimamizi na
udhibiti wa taka zenye madhara umebainishwa kwenye Vifungu vya 133 -139 vya
Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004. Pia Kanuni za Usimamizi wa
Mazingira (Usimamizi na Udhibiti wa Taka za Hatarishi) za Mwaka 2009 zimetoa
miongozo ya kudhibiti taka hatarishi hapa nchini pamoja na mambo mengine
yahusuyo uhifadhi wa mazingira.
Kwa muktadha huo, Ofisi ya Makamu wa Rais
inawaagiza watu wote wenye leseni za kukusanya taka hatarishi ikiwemo Vyuma Chakavu,
Betri zilizotumika na Taka za Kielektroniki kuwa, wapeleke leseni zao halisi
(Original Certificates) katika Ofisi za Kanda za Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC) zilizopo karibu yao kwa ajili ya uhakiki. Leseni
ambazo hazitahakikiwa kufikia tarehe 02/04/2019 zitakuwa Zimefutwa.
Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inatoa wito kwa
wananchi wote kuwa mtu yeyote atakayejihusisha na ununuaji au uuzaji wa vyuma
chakavu vinavyotokana na miundombinu ya taifa atashitakiwa kwa kosa la
uharibifu wa miundombinu chini ya sheria za uhujumu uchumi.
Mhandisi Joseph Malongo
KATIBU MKUU
       25 MACHI 2019
Anuani zimeambatanishwa kwa ajili ya rejea:
| 
Anorld Mapinduzi 
Meneja wa Kanda ya Kati 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
  Mazingira 
PSPF House 
Ghorofa ya sita 
Dodoma. | 
Jamal Baruti 
Meneja wa Kanda ya Ziwa 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
  Mazingira 
Ofisi  za
  Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Victoria, 
Igogo, Mwanza. | 
| 
Lewis Nzali 
Meneja wa Kanda ya Kusini 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
  Mazingira 
Tanu Road  
Mtwara. | 
Novertus Mushi 
Meneja wa Kanda ya Kaskazini 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
  Mazingira 
Engira Road, NHC Plot # 32 
Arusha. | 
| 
Jaffer Chimgege 
Meneja wa Kanda ya Mashariki 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
  Mazingira 
Regent Estate 
Plot # 29/30 
Dar es Salaam. | 
Godlove Mwamsojo 
Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
  Mazingira 
Karume Avenue 
Mbeya. | 
Post A Comment: