Naibu Waziri wa Maliasili  na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiweka shada kwenye kaburi la Mwl.Julius Kambarage Nyerere wakati wa ziara aliyoifanya katika makazi ya Baba wa Taifa wilayani Butiama mkoani Mara. Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Butiama, Mhe.Annarose Nyamubi
Naibu Waziri wa Maliasili  na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa pamoja na  mkuu wa wilaya ya Butiama, Mhe.Annarose Nyamubi mara baada ya kuweka shada la maua  kwenye kaburi la Mwl.Julius Kambarage Nyerere wilayani Butiama mkoani Mara.
 Naibu Waziri wa Maliasili  na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa pamoja na  mkuu wa wilaya ya Butiama, Mhe.Annarose Nyamubi mara baada ya kuweka shada la maua  kwenye kaburi la Mwl.Julius Kambarage Nyerere wilayani Butiama mkoani Mara.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiangalia picha ya Baraza la mwisho  la mawaziri mara baada ya kabla ya kuachia madaraka  wakati alipotembelea Makumbusho ya Mwl.Nyerere wilayani Butiama mkoani Mara
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiangalia huku akipewa maelezo kutoka kwa Afisa Mambokale, Baraka Bwire  orodha yaNwapigania uhuru wa Tanganyika  iliyochongwa kwenye mti wakati alipotembeleaMakumbusho ya Mwl.Nyerere wilayani Butiama mkoani Mara
Naibu Waziri wa Maliasili  na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya pamoja na watumishi wa
makumbusho ya  Mwl.Julius Kambarage Nyerere wakati Naibu Waziri huyo
alipotembelea Makumbusho hiyo . Wa tano kulia  ni mkuu wa wilaya ya
Butiama, Mhe.Annarose Nyamubi
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe.Constantine Kanyasu amesema Wizara kupitia Taasisi zake imejipanga kukikarabati na kukiendesha Kituo cha Makumbusho ya Mwalimu Nyerere, kwenye makazi ya Baba wa Taifa wilayani Butiama mkoani Mara.

 Amesema hatua hiyo inalenga kukiboresha kituo hicho ili kiweze  kuwavutia watalii wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kituo hicho wilayani Butiama mkoani Mara,  Mhe. Kanyasu amesema Makumbusho hiyo  ni hazina ya Taifa kutokana na uwepo wa mikusanyo na historia iliyobeba taswira ya Taifa la Tanzania kabla na baada ya Uhuru.

Amesema yeye akiwa Naibu Waziri  atahakikisha Makumbusho hiyo inatengewa bajeti ya kutosha ili kuiwezesha kuwa ya kisasa na yenye kuwavutia watalii.

Ameeleza  kuwa nchi mbalimbali duniani ikiwemo China zimekuwa zikiingiza fedha nyingi kupitia Makumbusho za viongozi ambao walikuwa  waasisi wa nchihizo kama alivyokuwa Mwl.Nyerere.

Amesema sifa aliyokuwa nayo Mwl. Julius Kambarage Nyerere lazima iakisi Makumbusho yake kwa kuwa bora na yenye kuwavutia watalii.

Makumbusho hiyo lazima iwekewe mazingira mazuri ili  iakisi utu na uzalendo wake kwa taifa la Tanzania.

 Aidha, amesema Makumbusho hiyo itafanyiwa utaratibu wa kuwa na watumishi wa kutosha wa kuihudumia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Makumbusho hiyo, Emamuel Kiondo  amemweleza Naibu Waziri huyo kuwa  kituo hicho kina watumishi wawili pekee walioajiriwa na  wengine wakiwa  watumishi wa kujitolea.

Aidha, ameeleza kuwa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo ya uhaba wa vitendea kazi.
Share To:

Post A Comment: