Kamati ya Bunge, Mifugo,  Kilimo na Maji imempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro kutokana na jitihada zake anazozionyesha zakuwasaidia wananchi Wa wilaya hiyo.

Hayo yamejiri kwenye ziara ya kamati hiyo  wilayani Arumeru  Mkoani Arusha baada ya kamati ya Bunge Mifugo, Kilimo na Maji kufanya ziara yakukagua miundo mbinu ya maji inayoendelea kujengwa  pamoja na Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji mifugo kwa njia ya chupa NAIC Kilichopo Wilayani Arumeru.

Akizungumza mara baada ya kukagua Miradi hiyo ya Maji Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Eng. Emmanuel Kalobelo amesema amefurahishwa na utendaji wa kazi wa DC  Muro kutokana na umakini na ufuatiliaji wa miradi mingi ya Maji  inayoendelea katika wilaya yake.

"Nashukuru kwa maelezo ya Mhe. Mkuu wa Wilaya ambaye tangu asubuhi ameonyesha jinsi gani anavyofuatilia miradi yote ndani ya wilaya yake, na anafahamu takwimu zote za miradi na stegi zilizofikiwa hivyo Mimi kama mtu wa sekta ya maji nimefarijika kweli na uongozi wa Wilaya ya Arumeru." Alisema Naibu Emmanuel Kalobelo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo ya bunge Ndugu Mahamoud Mgimwa amesema DC Muro anaitaji pongezi na kuungwa mkono  kutokana na juhudi zake anazoonyesha zakuwaletea wananchi wake maendeleo.

"Mhe Muro hapa anafanya kazi nzuri kuna kazi nyingine ambazo so za kwake lakini anajitolea,naomba tumpongeze sana, unawezajiuliza anafanya kwa ajili ya nani? Lakini ameamua kufanya kwa ajili ya kuwasaidia nyinyi ndugu zake, kwa zile juhudi anazozifanya mkuu wa wilaya na waombeni sana mumuunge  mkono." Alisema Mahamoud"


Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
21/03 /2019
Share To:

msumbanews

Post A Comment: