Saturday, 3 November 2018

SERIKALI YATAKA UNESCO KUTOA TAKWIMU ZA MAUAJI KWA NCHI BADALA YA JUMLA

IMG_20181102_134752
Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake nchini Tamwa Bi Edda Sanga akiongea na vyombo vya habari kwenye mkutano  wa waandishi wa habari kujadili hali ya usalama wawapo kazini uliondaliwa na shirika la Umoja wa mataifa la Elimu sanyansi na Utamaduni UNESCO kuandimisha siku ya kutathmini vitendo vya unyanyasaji na mauaji dhidi ya waandishi wa habari duniani ulifanyika jijini Arusha IMG_20181102_134004
Waziri wa Habari sanaa Michezi na Utamaduni Dkta.Harrison Mwakyembe akiongea na vyombo vya habari baada ya kuzindua mkutano wa waandishi wa habari kujadili hali ya usalama wawapo kazini uliondaliwa na shirika la Umoja wa mataifa la Elimu sanyansi na Utamaduni UNESCO kuandimisha siku ya kutathmini vitendo vya unyanyasaji na mauaji dhidi ya waandishi wa habari duniani ulifanyika jijini Arusha
…………………………
Na Ahmed Mahmoud Arusha
SERIKALI  imelitaka shirika la kimataifa ,Elimu ,Sayansi na Uchumi (UNESCO)kutoa takwimu sahihi juu ya matukio ya waandishi wa habari kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji na mauaji kwa kila nchi tofauti na kutoa takwimu za jumla ili kuangalia ukubwa wa jambo hilo kwa kila taifa.
Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Dkt ,Harrison Mwakyembe ameyasema hayo katika mkutano wa kimataifa unaowashirikia waandishi wa habari kutoka nchi za ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara (SADC)katika siku ya kutathmini vitendo vya unyanyasaji na mauaji dhidi ya waandishi wa habari dunia uliondaliwa na Unesco jijini hapa.
Amesema takwimu zilizotolewa na UNESCO zinazoonyesha kuwa waandishi wa habari wapatao 1010 waliuawa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita,jambo ambalo halifafanui kiwango cha ukubwa kwa Kila nchi zilizokumbwa na Kadhia hiyo .
Insert Dkt.Mwakyembe
Aidha amesema kuwa Umoja wa mataifa umetenga siku ya Tarehe 2 kila mwaka kuadhimisha siku ya kupinga vitendo vya unyanyasaji,uzalilishaji na mauaji kwa wanahabari kote ulimwenguni lakini matatizo hayo yamekuwa yakijirudia bila kuyapatia ufumbuzi jambo ambalo ametaka takwimu za kila nchi zikabainishwa ikujua uwiano ili kupima ukubwa wa tatizo.
Awali akiongea kwenye mkutano huo Mkurugenzi wa Unesco Kanda ya Afrika mashariki Johnbosco Mayiga amesema kuwa katika kipindi cha miaka kumi jumla ya wanahabari wapatao 1010 waliuawa katika nchi mbali mbali duniani na hivyo kuongeza ukubwa wa vitendo vya ukatili kwa wanahabari kukosa uhuru na usalama wawapo katika utekelezaji majukumu yao.
Katika Mkutano wa Unesco uliofanyika mwaka jana jijini Nairobi uliazimia kila nchi kuangalia utaratibu gani wa kufanya ili kuwajengea mazingira mazuri ya utendaji kazi kwa waandishi wa habari ikiwemo kuwa na chombo cha kuwalinda.
Pamoja na Mambo mengine mkutano huu utalenga kuangalia utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa Nairobi ikiwemo ni hatua zipi ziweze kuchukuliwa katika kuhakikisha muandishi wa habari anatekeleza majukumu yake katika mazingira salama.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (Tamwa) Bi Edda Sanga amesema kuwa kitu alichokipenda katika mkutano huo ni mgawanyo wa  wa wajumbe na kuwa mwandishi si elimu pekee na ujuzi wa kazi utakaosaidia utendaji kazi wake
Amesema kuwa vyombo vya habari vina nguvu kubwa ya kutupeleka katika hatua kubwa ya maendeleo iwapo kutakuwa na mazingira mazuri kwa wanahabari na kutekeleza majukumu yao kwa weledi .

No comments:

Post a comment