Tuesday, 11 September 2018

"MWENGE WA UHURU"JUMLA YA MIRADI 22 KUZINDULIWA ARUSHA


Mkuu wa mkoa wa arusha Mrisho Gambo kwa ushirikiano na wakuu wa wilaya mkoani humo wanatarajiwa kupokea Mwenge wa uhuru septemba 12 wilayani Ngorongoro ukitokea mkoani Mara.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa baada ya kuupokea mwenge huo viongozi wa mwenge wanatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya sita za mkoa wa arusha.

Baadhi ya miradi itakayo zinduliwa ni miradi kwa ajili ya kuboresha Sekta ya afya,Elimu,pamoja na miundo mbinu ya barabara kuelekea tanzania ya viwanda.
"Serikali tayari imeshatoa kiasi cha shilingi *7,416,735,688.35* kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla"
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: