Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel(kulia) akichanganya mchanga na saruji kuashiria ujenzi wa Shule ya Kiingereza katika eneo la Bomba Mbili Mjini Geita.Akishiriki Zoezi hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita Bw Richard Jordinson
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel(kulia) akichanganya mchanga na saruji kuashiria ujenzi wa Shule ya Kiingereza katika eneo la Bomba Mbili Mjini Geita.Akishiriki Zoezi hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita Bw Richard Jordinson
Jumamosi Septemba 8 2018, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi . Robert Gabriel amezindua awamu nyingine ya miradi inayofadhiliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGML) pamoja na Halmashauri za Wilaya na Mji wa Geita   chini ya Mpango wa fedha za Miradi ya huduma kwa jamii kwa mawaka 2018.

Uzinduzi wa Miradi katika awamu hii unahusisha ujenzi wa Kiwanda cha Alizeti, Zahanati,madarasa manne na nyumba  nne za watumishi wa Afya kwenye vijiji vya Nyakabale, Manga, Ikulwa , Ihanamilo, Buhalala,Magaenge pamoja na Kasota ndani ya Wilaya ya Geita.

Uzinduzi huo utahusisha pia ukabidhiwaji wa Kituo cha Polisi Jamii katika kijiji cha Nyakabale pamoja na Trekta jipya kwenye kikundi cha ushirika cha NYABUSAKAMA kinachoundwa na vijiji vya Saragulwa Nyakabale, Bugulula, Saragulwa, Kasota pamoja na Manga.

Mkurugenzi Mtendaji wa GGML Bwana. Richard Jordinson amesema kuwa uzinduzi wa kuanza kwa  ujenzi wa Miradi hiyo ya kihistoria ni mwanzo wa maendeleo ya jamii mjini Geita na kwamba shughuli za uchimbaji zinazofanywa na Kampuni hiyo ni kwa ajili ya kuchochea maendeleo endelevu ya uchumi kwa faida ya wakazi wa  Mkoa wa Geita na Tanzania kwa ujumla.

"Tunafurahi kuona kwamba, GGML kama Kampuni raia,inaendelea kuleta manufaa kwa jamii inayozunguka Mgodi. Utekelezaji wa miradi hii ni moja ya ushuhuda wa wazi kwamba GGML, Serikali na Jamii  inayotuzunguka inaweza kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuboresha miundombinu na huduma bora za jamii, "alisema.

Bw Jordinson ametambua na kupongeza mchango na ushirikiano unaotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na Serikali za mitaa katika utekelezaji wa miradi ya CSR, akielezea: "Kampuni ingependa kutoa Shukrani zake za dhati kwa Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wote wa Halmashauri ya Mji na Wilaya  kwa msaada na uongozi wao katika utekelezaji wa Miradi hiyo.”

Gharama yote katika utekelezaji wa Miradi inayofadhiliwa na GGML chini ya Mpango wa CSR kwa mwaka 2018, ni shilingi za Kitanzania  bilioni 9.2 ambazo zitatekeleza miradi mingi ikiwemo ufungaji wa taa za barabarani zinazotumia mwanga wa Jua katika barabara kuu za mji wa Geita, ujenzi wa mnara katika makutano ya barabara za Mji wa Geita pamoja na ujenzi wa soko la kisasa katika Mji wa Geita.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: