Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Monduli Mjini, Isack Joseph amejiuzulu nafasi hiyo, kujivua uanachama na kukihama chama hicho kisha kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Isack na viongozi wengine zaidi ya 31 wa ngazi ya Wilaya na Kata wamejiunga na CCM  jana  Agosti 11, 2018 ikiwa ni wiki chache baada ya aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Monduli, Kalanga kuhamia CCM. Viongozi hao wamepokelewa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: