Tuesday, 14 August 2018

Muuza mitumba akabidhiwa gari na Diamond Platnumz

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye pia ndiye mkurugenzi wa WCB amemkabidhi gari mshindi wa shindano la Nogewa Ushinde lililokuwa likifanyika kwa mwezi mmoja sasa kupitia bidhaa za Diamond Karanga.

Mshindi huyo aliyejitambulisha kwa majina ya Bakari Saidi akisimulia kwa furaha amesema kuwa yeye ni muuza mitumba Ubungo jijini Dar es salaam na ameahidi kuendelea kutumia bidhaa hizo huku akidai kwamba gari hilo limemkomboa kiuchumi.

No comments:

Post a Comment