Friday, 20 July 2018

WAZIRI MHAGAMA AITAKA NSSF KUIFIKIA SEKTA ISIYO RASMI NCHINI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea na wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu akifafanua jambo wakati wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ( wa kwanza) akifuatilia kikao, wakati wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakifuatilia kikao wakati walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, jijini Dar es Salaam.

……………………

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) amelitaka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuwa na mkakati utakaoliwezesha Shirika hilo kuifikia sekta isiyo rasmi ili kuwezesha shirika hilo kupanua wigo wa hifadhi ya Jamii na kukusanya michango itakayowezesha shirika kulipa mafao kwa wakati na kufanya shughuli za uwekezaji nchini.

Akizungumza na wajumbe wa Bodi na menejimenti ya NSSF jana tarehe 18 Julai 2018, jijini Dar es Salaam, Mhe. Mhagama alifafanua kuwa sekta isiyo rasmi ni moja ya sekta ambayo haijafikiwa na hifadhi ya jamii kwa kiwango cha kuridhisha, hivyo NSSF haina budi kuhakikisha kuwa sekta hiyo inafikiwa kwa kiwango kikubwa.

“Mfuko huu pamoja na mambo mengine umepewa jukumu la kusimamia sekta isiyo rasmi na katika sekta ambazo hazijafikiwa na hifadhi ya jamii kwa mujibu wa ibara ya 11 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni pamoja na sekta isiyo rasmi, hakikisheni mnaifikia sekta hiyo, hamuwezi kufanya uwekezaji katika miradi bila kuwa na wanachama wanaochangia mfuko ” Amesema Mhagama.

Katika mkutano huo, Mhe. Mhagama alimtambulisha Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii, Bw. William Erio, na kumtaka Mkurugenzi huyo kusimamia kwa weledi shuhghuli za uwekezaji zinazofanywa na NSSF nakuhakikisha mradi wa Mkulazi unafikia malengo na unazalisha sukari kama ilivyokusudiwa.Mhe. Mhagama amemtaka Mkurugenzi huyo kufikia maamuzi ya mwisho kuhusu mradi wa Dege na kufanya mapitio ya miradi yote na kuona hali halisi ilivyo na kufanya maamuzi stahiki na kuleta tija kwa wanachama na taifa.

‘’Mkurugenzi uendelea kulinda fedha za wanachama na kulipa mafao kwa wakati. lakini Bodi pamoja na menejimenti ya NSSF, mpeni ushirikiano Mkurugenzi huyu na fanyeni kazi kwa uadilifu na uzalendo ili kuweza kuhakikisha kuwa mfuko huu unakuwa na tija kwa wanachama na kujenga uchumi wa nchi” Amesema Mhagama.

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilianzishwa chini ya sheria Na. 28 ya mwaka 1997 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sura Na. 50 na Sheria ya pensheni kwa watumishi wa umma Na. 2 ya mwaka 2018.

No comments:

Post a comment