NAIBU wa Waziri ya Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, amesema kuwa vyuo vya elimu vizalishe wahitimu  wenye sifa ambao watakuwa mchango katika uchumi wa viwanda kwa vilivyopo na vitakavyoanzishwa.

Serikali haitegemei watalaam kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuendesha viwanda wakati vyuo vipo na vinazalisha watihimu kila siku.Ole Nasha aliyasema hayo wakati akifunga maonesho ya 13 ya vyuo vikuu nchini na Nje ya Nchi yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Amesema katika vyuo hivyo vinatakiwa kuwaandaa vijana ili waweze kupata stadi na ujuzi stahiki na isiwe bora elimu bali elimu bora kwa nia ya kuelekea uchumi wa viwanda kutokana na dhamira ya serikali ya awamu ya tano chini Dk. John Pombe Magufuli.

Naibu  Waziri huyo, amesema serikali haitavumilia taasisi au mtu yoyote anayejaribu kukiuka miongozo ya uanzishaji wa vyuo visivyo na ubora hatabaki salama ni bora kuwa na vyuo vichache vyenye sifa stahiki na koundoa utitili wa vyuo ambao havina ubora.

‘’Nitoe msisitizo kwa taasisi zote za elimu ya juu ambazo zilihakikiwa na kubainika kuwa zina mapungufu mbalimbali zijirekebishe kasoro hizo mapema iwezekanavyo kwa kuzingatia maelekezo ya Mamlaka husika zinazosimamia ubora wa elimu ya juu, yaani Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE),’’alisema.

Amesema serikali ina mategemeo makubwa ya kupata wahitimu wenye ujuzi unaotakiwa kwenye uchumi wa viwanda.Mwenyekiti wa Bodi  wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Jacob Mtabaji, amesema maonyesho hayo yamewafanya kukutana na taasisi mbalimbali ambazo simewasaidia kubadilishana uzoefu.

Profesa Mtabaji, amesema maonyesho haya wanategemea kupata wahitimu wenye maadili mema na mahitaji  ambao ni halisi kwa soko.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: