Friday, 20 July 2018

Mama Salma Kikwete afiwa na Baba yake mzazi


MKE wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum (CCM) amepata pigo kwa kuondokewa na baba yake mzazi, Mzee Rashid Mkwachu leo Alhamisi, Julai 19, 2018.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mjukuu wa marehemu ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, msiba huo upo nyumbani kwa Dkt. Jakaya Kikwete maeneo ya Msasani jijini Dar es Salaam na mazishi yatafanyika kesho Ijumaa, Julai 20, 2018 katika Makaburi ya Kisutu majira ya saa 10:00 jioni.

No comments:

Post a Comment