Sunday, 15 July 2018

Madiwani wa Chadema Morogoro wasusia uchaguzi mdogo wa Naibu Meya

Madiwani wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema katika halmashauri ya manispaa ya morogoro na mbunge wa viti maalum  kupitia chama hicho mheshimiwa devotha minja wamesusia uchaguzi mdogo wa baraza la madiwani kumchagua naibu meya wa manispaa hiyo kwa madai ya kuwa uchaguzi  huo haukuwa wa haki kwa kutangaza jina moja la mgombea kutoka chama cha mapinduzi ccm.

Awali kabla ya uchaguzi huo wa naibu meya kuanza madiwani wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema wamestushwa na kitendo cha kusomwa jina la mgombea wa chama cha mapinduzi ccm pekee na kulazimika kuomba muongozo.

Hata hivyo baada ya kuomba muongozo na kukataliwa madiwani hao walitoka nje na kususia uchaguzi huo ambapo wakiwa nje ya ukumbi wa halmashauri akiwemo mbunge huyo ameleza waandishi wa habari kilicho sababisha kutoka na kususia uchaguzi huo.

Kwa upande wake mkurugenzi  mtendaji wa  halmashauri  ya manispaa ya morogoro john  mgalula anaelezea utaratibu wa uchaguzi huo ulivyokua huku nafasi hiyo ya unaibu meya ikichukuliwa na mgombea wa chama cha mapinduzi ccm.

No comments:

Post a Comment