Thursday, 19 July 2018

Lowassa, Zitto Kabwe Wakutana Faragha

Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe wamekutaka na kufanya mazungumzo leo Alhamisi Julai 19, 2018.

Taarifa iliyotolewa leo na msaidizi wa waziri mkuu huyo, Aboubakary Liongo imesema katika mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisini kwa Lowassa,  viongozi hao walijadiliana juu ya mwenendo wa hali ya siasa Tanzania na mchango wa vyama vya siasa kwenye maendeleo ya nchi.

Taarifa hiyo iliyoambatana na picha zinazowaonyesha wawili hao wakijadiliana masuala mbalimbali, haikueleza kiundani walichozungumza.

No comments:

Post a Comment