Nanji alibwaga manyanga jana wakati Pole pole akimnadi mgombea wa CCM Elirehema Nnko ambapo alikunwa na utekelezaji wa ilani na kuamua kupanda jukwaani na kusalimisha nyaraka zake zote ikiwemo kadi yake ya uanachama wa ACT.

Kujiuzulu kwa diwani huyo kuliibua shangwe na nderemo na vifijo kwa wananchama wa CCM waliokuwa wamefurika katika viwanja vya  Bullet vilivyoko katika kata ya Osunyai baada ya Nanji kubwaga manyanga.

Akizungumza  mara baada ya kupokelewa na Pole Pole Nanji alisema utekelezaji wa Ilani ya CCM uliotolewa na Pole Pole umemkuta akiamua kujiuzulu nafasi yake ya kugombea udiwani kupitia ACT kwa kuwa haina ilani yeyote na CCM ndiyo chama dume ambacho ilani yake inatekelezeka kwa vitendo.

"Nashukuru CCM kunipokea nilikiwa utumwani Misri lakini sasa nimerudi nyumbani Kaanani nchi iliyojaa asali na maziwa na uwezo wa kutembea kifua mbele tofauti na awali nivyokuwa natembea kwa kijificha".

Licha ya mgombea huyo pia diwani wa kata  Machame Uroki Robnson Kimaro(CHADEMA)  kutoka halmashauri ya wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro  naye alijiuzulu wadhifa wake wa udiwani na kujiunga na CCM mbele ya Pole Pole

Naye Kimaro alisema ameamua kurudi CCM kutokana na CCM kuwa na ilani inayotekelezeka kwa vitendo lakini pia utendaji kazi mzuri wa rais Dk John Magufuli.

Aidha wafuasi wa CHADEMA na ACT waliokiwa katika mkutano huo wa kampeni zaidi ya 20 pia walibwaga manyanga na kujiunga na CCM.

Kujiuzulu kwa mgombea huyo wa ACT ambaye alikuwa anachuana na Nnko kumemwezesha mgombea huyo wa CCM kupita bila kupingwa ambapo sasa anasubiri kuapishwa baada ya uchaguzi wa Agosti 12 mwaka huu.









Share To:

msumbanews

Post A Comment: