Thursday, 19 July 2018

Irene Uwoya na Hamissa Mobetto Waomba radhi Kwa Picha za Nusu Uchi Kama Walivyoagizwa na TCRA

Wasanii Hamisa Mobeto na Irene Uwoya wameomba radhi kwa kosa la kuweka picha za utupu katika mitandao ya kijamii. Wamechukua uamuzi huo saa chache baada ya kutakiwa kufanya hivyo na kamati ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano (TCRA).

Uamuzi wa TCRA umetolewa leo asubuhi Alhamisi Julai 19, 2018 baada ya wasanii hao kukiri kosa katika mkutano uliowahusisha waandishi wa habari.

Kupitia kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Instagram, Uwoya ndio alikuwa wa kwanza kuomba radhi kwa kuweka picha anayoonekana amejilaza huku sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi.

“Wapenzi wangu, ndugu zangu, wakubwa zangu na wadogo zangu naomba radhi kwa picha niliyopost ...,najua nimekwaza, sikujua nitawakwaza sababu ya role mode wangu Beyonce, nimejifunza sasa …,nawapenda,"

Naye Hamissa ameandika….

NAOMBA RADHI KWA UMMA:

Husika Na Kichwa Cha Habari Hapo Juu.

Mimi Hamisa Mobetto
Ambaye ni Mfanya Biashara Wa Mitindo (Fashion Entrepreneur) Apa Nchini Tanzania Na Pia Ni Raia Wa Tanzania 🇹🇿 Naomba Kutumia Fursa Hii Kuomba Radhi Kwa Watanzania na Wengine Wote Ambao Ni Watumiaji Wa Mitandao .
Kuhusiana Na Kitendo Cha Mimi Na Washabiki Zangu (Fans) Wangu Kutuma Picha Zangu Zinazoonyesha Nusu Utupu Kwenye Page Zao Za Instagram.
.
Pia Natumia Fursa Hii Kuwashukuru Kamati Ya Maudhui Kwa Jinsi Walivyonita Kwenye Kamati Yao Na Kunipa Nafasi Ya Kujitetea Na Mwisho Kufanya Uamuzi Wenye Haki Kwangu Na Kwa Wapenzi (fans) Wangu Wote . Ninawashukuru Sana.🙏🏾
.
Mwisho Kabisa Niwahusie Vijana Wenzangu Kuepuka Kutumia Mitandao Ya Kijamii vibaya Kwani Kwa Sasa Kuna Sheria Kali Zinazokataza Picha Mbaya kutumwa Kwenye Mitandao .Naomba Pia Wapenzi (fans)Wangu Kuanzia Sasa Kutuma Picha Zangu Zenye Staha Au Kutumia Biashara Zangu Kunisapoti.
.
Nawashakuru Sana Na Mbarikiwe Sana.❤️🙏🏾

No comments:

Post a comment