Thursday, 19 July 2018

Gari la kubeba wagonjwa lapata ajali

Gari la kubeba wagonjwa la Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu limepata ajali, huku ndani likiwa na matairi chakavu tisa.

Ajali hii imetokea siku chache baada ya serikali kupiga marufuku magari hayo ya wagonjwa kupakia kitu chochote zaidi ya wagonjwa.

Huko mkoani mara gari la wagonjwa lilikamatwa siku chache zilizopita likiwa limebeba madawa ya kulevya aina ya mirungi na kusababisha watumishi kusimamishwa kazi.

No comments:

Post a comment