Monday, 16 July 2018

WAWAKILISHI WA WANANCHI WAMEASWA KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI KUFIKISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO


Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Wanahabari Tanzania " Union of Tanzania Press Club" imeasa wawakilishi wa Wananchi kuiga mfano wa  Mbunge Jimbo la Nyamagana kuifikishia jamii habari ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi au Miradi ya maendeleo kupitia Vyombo vya habari. 

Hayo yamebainishwa na  Victor Maleko kaimu Mkurugenzi wa Umoja wa Vilabu Vya Waandishi wa Habari Tanzania katika Ziara ya Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula katika ofisi yao  UTPC hivi leo. Ndg Maleko amempongeza Mhe Mabula kuwa amekuwa kiongozi wa mfano kuchukua hatua kufikia taasi za habari ikiwemo UTPC. Amewaasa viongozi mbali mbali kufuata nyao hiyo sanjari kutumia vyama vya waandishi wa habari katika kuratibu shughuli za habari maana vipo kila mkoa nchini.

Kadharika Mhe Mabula ameipongeza UTPC kwa harakati za kuwaunganisha Vyama Vya waandishi wa habari mikoa yote nchini Tanzania. "Ninafarijika kuona taasis hii ina simama imara katika kuratibu mafunzo pamoja na kutetea haki za waandishi,  nina ahaidi kuendeleza mahusiano na taasi za habari kwa mstakabali wa ujenzi wa taifa." Mhe Mabula alisema.

Mbunge Jimbo la Nyamagana amekabidhiwa machapisho ya UTPC pamoja na Jarida la Tuwasiliane yanayoandiliwa na taasis hiyo. Ziara hii ya Mhe Mabula  katika Vyombo Vya habari  imeanza  leo tarehe 16.07.2018 na itaisha kesho kutwa Ijumatano tarehe 18.07.2018.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge 
Jimbo la Nyamagana🇹🇿

No comments:

Post a Comment